Yeremia 42:5-6
Yeremia 42:5-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Kisha, watu wakamwambia Yeremia, “Mwenyezi-Mungu na awe shahidi wa kweli na mwaminifu dhidi yetu ikiwa hatutafanya jinsi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako atakavyokuagiza utuambie. Iwe ni jambo la kupendeza au la, sisi tutaitii sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu ambaye tunakutuma kwake ili tufanikiwe tutakapomtii Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu.”
Yeremia 42:5-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wakamwambia Yeremia, BWANA na awe shahidi wa kweli na uaminifu kati yetu; ikiwa hatufanyi sawasawa na neno lile, ambalo BWANA, Mungu wako, atakutuma utuletee. Likiwa jema, au likiwa baya, sisi tutaitii sauti ya BWANA, Mungu wetu, ambaye tunakutuma kwake; ipate kuwa faida yetu, tunapoitii sauti ya BWANA, Mungu wetu.
Yeremia 42:5-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wakamwambia Yeremia, BWANA na awe shahidi wa kweli na uaminifu kati yetu; ikiwa hatufanyi sawasawa na neno lile, ambalo BWANA, Mungu wako, atakutuma utuletee. Likiwa jema, au likiwa baya, sisi tutaitii sauti ya BWANA, Mungu wetu, ambaye tunakutuma kwake; ipate kuwa faida yetu, tunapoitii sauti ya BWANA, Mungu wetu.
Yeremia 42:5-6 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kisha wakamwambia Yeremia, “BWANA na awe shahidi wa kweli na mwaminifu kati yetu kama hatutafanya sawasawa na kila kitu BWANA Mungu wako atakachokutuma utuambie. Likiwa jema au likiwa baya, tutamtii BWANA Mungu wetu, ambaye tunakutuma kwake, ili mambo yote yawe mema kwetu, kwa maana tutamtii BWANA Mungu wetu.”