Yeremia 42:21-22
Yeremia 42:21-22 Biblia Habari Njema (BHN)
Leo mimi nimewaambieni lakini hamkutii chochote ambacho Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu amenituma niwaambie. Basi, jueni hakika kwamba mahali mnapotamani kwenda kukaa mtafia hukohuko kwa vita, njaa na maradhi.”
Yeremia 42:21-22 Swahili Revised Union Version (SRUV)
nami nimewafunulia haya leo; lakini ninyi hamkuitii sauti ya BWANA, Mungu wenu, katika neno lolote ambalo amenituma kwenu. Basi, sasa jueni sana ya kuwa mtakufa kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni, katika mahali pale mnapopatamani kwenda na kukaa.
Yeremia 42:21-22 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
nami nimewafunulia haya leo; lakini ninyi hamkuitii sauti ya BWANA, Mungu wenu, katika neno lo lote ambalo amenituma kwenu. Basi, sasa jueni sana ya kuwa mtakufa kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni, katika mahali pale mnapopatamani kwenda na kukaa.