Yeremia 4:27-28
Yeremia 4:27-28 Biblia Habari Njema (BHN)
Maana Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Nchi nzima itakuwa jangwa tupu; lakini sitaiharibu kabisa. Kwa hiyo, nchi itaomboleza, na mbingu zitakuwa nyeusi. Maana, nimetamka na sitabadili nia yangu; nimeamua, wala sitarudi nyuma.
Yeremia 4:27-28 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Maana BWANA asema hivi, Nchi yote itakuwa ukiwa; lakini sitaikomesha kabisa. Kwa ajili ya hayo nchi itaomboleza, na mbingu zitakuwa nyeusi; kwa sababu mimi nimeyanena haya, na kuyakusudia, wala sikujuta wala mimi sitarudi nyuma niyaache.
Yeremia 4:27-28 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)