Yeremia 23:13-14
Yeremia 23:13-14 Biblia Habari Njema (BHN)
“Miongoni mwa manabii wa Samaria, nimeona jambo la kuchukiza sana: Walitabiri kwa jina la Baali wakawapotosha watu wangu Waisraeli. Lakini miongoni mwa manabii wa Yerusalemu, nimeona kinyaa cha kutisha zaidi: Wanafanya uzinzi na kusema uongo; wanawaunga mkono wanaotenda maovu hata pasiwe na mtu anayeachana na uovu. Kwangu wote wamekuwa kama watu wa Sodoma; wakazi wake wamekuwa wabaya kama watu wa Gomora.
Yeremia 23:13-14 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nami nimeona upumbavu katika manabii wa Samaria; walitabiri kwa Baali, wakawakosesha watu wangu Israeli. Katika manabii wa Yerusalemu nimeona neno linalochukiza sana; hufanya zinaa; huenda katika maneno ya uongo, hutia nguvu mikono ya watendao maovu, hata ikawa hapana mtu arejeaye na kuuacha uovu wake; wote pia wamekuwa kama Sodoma kwangu, na wenyeji wake kama Gomora.
Yeremia 23:13-14 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nami nimeona upumbavu katika manabii wa Samaria; walitabiri kwa Baali, wakawakosesha watu wangu Israeli. Katika manabii wa Yerusalemu nimeona neno linalochukiza sana; hufanya zinaa; huenenda katika maneno ya uongo, hutia nguvu mikono ya watendao maovu, hata ikawa hapana mtu arejeaye na kuuacha uovu wake; wote pia wamekuwa kama Sodoma kwangu, na wenyeji wake kama Gomora.
Yeremia 23:13-14 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Miongoni mwa manabii wa Samaria nililiona jambo la kuchukiza: Walitabiri kwa Baali na kuwapotosha Israeli watu wangu. Nako miongoni mwa manabii wa Yerusalemu nimeona jambo baya sana: Wanafanya uzinzi na kuenenda katika uongo. Wanatia nguvu mikono ya watenda mabaya, kwa ajili hiyo hakuna yeyote anayeachana na uovu wake. Wote wako kama Sodoma kwangu; watu na Yerusalemu wako kama Gomora.”