Isaya 66:20
Isaya 66:20 Biblia Habari Njema (BHN)
Watawarejesha ndugu zenu wote kutoka katika mataifa yote kama matoleo yangu mimi Mwenyezi-Mungu. Watawaleta wamepanda farasi, nyumbu, ngamia na magari ya farasi mpaka Yerusalemu, kwenye mlima wangu mtakatifu. Watawaleta kama Waisraeli waletavyo sadaka ya nafaka katika chombo safi hadi nyumbani kwangu mimi Mwenyezi-Mungu.
Isaya 66:20 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nao watawaleta ndugu zenu wote kutoka mataifa yote, kuwa sadaka kwa BWANA, juu ya farasi, na katika magari, na katika machela, na juu ya nyumbu, na juu ya wanyama wepesi, mpaka mlima wangu mtakatifu Yerusalemu, asema BWANA; kama vile wana wa Israeli waletavyo sadaka yao nyumbani kwa BWANA katika chombo safi.
Isaya 66:20 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nao watawaleta ndugu zenu wote kutoka mataifa yote, kuwa sadaka kwa BWANA, juu ya farasi, na katika magari, na katika machela, na juu ya nyumbu, na juu ya wanyama wepesi, mpaka mlima wangu mtakatifu Yerusalemu, asema BWANA; kama vile wana wa Israeli waletavyo sadaka yao nyumbani kwa BWANA katika chombo safi.
Isaya 66:20 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Nao watawaleta ndugu zenu wote, kutoka mataifa yote, mpaka kwenye mlima wangu mtakatifu katika Yerusalemu kama sadaka kwa BWANA, juu ya farasi, katika magari ya vita na magari makubwa, juu ya nyumbu na ngamia,” asema BWANA. “Watawaleta, kama Waisraeli waletavyo sadaka zao za nafaka, katika Hekalu la BWANA, katika vyombo safi kwa kufuata desturi za ibada.