Ezra 5:9-10
Ezra 5:9-10 Biblia Habari Njema (BHN)
Tuliwauliza viongozi hao watuambie ni nani aliyewapa amri ya kuijenga upya nyumba hii mpaka kuimaliza. Tuliwauliza pia majina yao ili tuweze kukujulisha wale wanaoongoza kazi hiyo.
Ezra 5:9-10 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ndipo tukawauliza wale wazee, tukawaambia hivi, Ni nani aliyewapa amri kuijenga nyumba hii, na kuumaliza ukuta huu? Tukawauliza pia majina yao, ili kukuhakikishia, tupate kuandika majina ya watu waliokuwa wakubwa wao.
Ezra 5:9-10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ndipo tukawauliza wale wazee, tukawaambia hivi, Ni nani aliyewapa amri kuijenga nyumba hii, na kuumaliza ukuta huu? Tukawauliza pia majina yao, ili kukuarifu wewe, tupate kuandika majina ya watu waliokuwa wakubwa wao.