Kutoka 35:4-9
Kutoka 35:4-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Mose aliiambia jumuiya yote ya Waisraeli, “Hili ndilo jambo ambalo Mwenyezi-Mungu amewaamuru mlifanye: Mtatoa katika mali zenu mchango wa kumpa Mwenyezi-Mungu. Kila mtu mwenye moyo mwema atamletea Mwenyezi-Mungu mchango: Dhahabu, fedha, shaba; sufu ya buluu, ya zambarau na nyekundu; kitani safi iliyosokotwa; manyoya ya mbuzi; ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu, ngozi za mbuzi; mbao za mjohoro, mafuta kwa ajili ya taa, viungo kwa ajili ya mafuta ya kupaka na kwa ajili ya ubani wenye harufu nzuri; vito vya sardoniki na vito vingine kwa ajili ya mapambo ya kizibao na kifuko cha kifuani.
Kutoka 35:4-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kisha Musa akanena na mkutano wote wa wana wa Israeli, akawaambia, Neno hili ndilo aliloliamuru BWANA, akisema, Katwaeni kati yenu matoleo kwa BWANA; mtu yeyote aliye na moyo wa kupenda, ayalete matoleo; dhahabu na fedha na shaba; na nyuzi za rangi ya buluu, zambarau, nyekundu, na kitani nzuri, na singa za mbuzi; na ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu, ngozi za pomboo na mbao za mshita; na mafuta kwa hiyo taa, na viungo vya manukato kwa hayo mafuta ya kutiwa, na kwa huo uvumba mzuri; na vito vya shohamu, vito vya kutiwa kwa hiyo naivera na kwa hicho kifuko cha kifuani.
Kutoka 35:4-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kisha Musa akanena na mkutano wote wa wana wa Israeli, akawaambia, Neno hili ndilo aliloliamuru BWANA, akisema, Katwaeni kati yenu matoleo kwa BWANA; mtu awaye yote aliye na moyo wa kupenda, ayalete matoleo; dhahabu na fedha na shaba; na nyuzi za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na za rangi nyekundu, na kitani nzuri, na singa za mbuzi; na ngozi za kondoo waume zilizotiwa rangi nyekundu, na ngozi za pomboo, na mbao za mshita; na mafuta kwa hiyo taa, na viungo vya manukato kwa hayo mafuta ya kutiwa, na kwa huo uvumba mzuri; na vito vya shohamu, na vito vya kutiwa kwa hiyo naivera, na kwa hicho kifuko cha kifuani.
Kutoka 35:4-9 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Mose akaiambia jumuiya yote ya Waisraeli, “Hili ndilo BWANA aliloamuru: Toeni sadaka kwa BWANA kutoka mali mliyo nayo. Kila mmoja aliye na moyo wa kupenda atamletea BWANA sadaka ya dhahabu, fedha na shaba; nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, za rangi nyekundu na kitani safi; singa za mbuzi; ngozi za kondoo dume zilizopakwa rangi nyekundu, na ngozi za pomboo; mbao za mshita; mafuta ya zeituni kwa ajili ya taa; vikolezi kwa ajili ya mafuta ya upako, pamoja na uvumba wa harufu nzuri; vito vya shohamu, na vito vingine vya thamani vya kuweka kwenye kisibau na kile kifuko cha kifuani.