Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kutoka 35

35
Kanuni za Sabato
1 # Kut 34:32 Musa akakutanisha mkutano wote wa wana wa Israeli, na kuwaambia, Maneno aliyoyausia BWANA ni haya, kwamba myafanye. 2#Kut 20:8-11; 23:12; 31:15; 34:21; Law 23:3; Kum 15:12-14; Hes 15:32; Kum 5:12; Lk 13:14 Fanyeni kazi siku sita, lakini siku ya saba itakuwa siku takatifu kwenu; ni Sabato ya kustarehe kabisa kwa BWANA; mtu yeyote atakayefanya kazi yoyote katika siku hiyo atauawa. 3#Kut 16:23 Hamtawasha moto katika nyumba zenu kwa siku ya Sabato.
Maandalizi ya hema ya kukutania
4 # Kut 25:1,2 Kisha Musa akanena na mkutano wote wa wana wa Israeli, akawaambia, Neno hili ndilo aliloliamuru BWANA, akisema, 5#Kut 25:2; 2 Kor 9:7 Katwaeni kati yenu matoleo kwa BWANA; mtu yeyote aliye na moyo wa kupenda, ayalete matoleo; dhahabu na fedha na shaba; 6na nyuzi za rangi ya buluu, zambarau, nyekundu, na kitani nzuri, na singa za mbuzi; 7na ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu, ngozi za pomboo na mbao za mshita; 8na mafuta kwa hiyo taa, na viungo vya manukato kwa hayo mafuta ya kutiwa, na kwa huo uvumba mzuri; 9na vito vya shohamu, vito vya kutiwa kwa hiyo naivera na kwa hicho kifuko cha kifuani. 10#Kut 31:6; 1 Fal 7:14; Isa 28:26 Na kila mtu kati yenu aliye na moyo wa hekima na aje, na kuyafanya hayo yote ambayo BWANA ameyaagiza; 11#Kut 25:9; 26:1,2; 39:32-43; 40:2; Mdo 7:44,45; Ebr 8:2,5; 9:2-11; Ufu 21:3 yaani, hiyo maskani na hema yake, kifuniko chake, vifungo vyake, mbao zake, mataruma yake, viguzo vyake na vitako vyake; 12#Kut 25:10 hilo sanduku, miti yake, hicho kiti cha rehema na lile pazia la sitara; 13#Kut 25:23,30; Law 24:5,6 na hiyo meza, miti yake, vyombo vyake vyote na hiyo mikate ya wonyesho; 14#Kut 25:31 na hicho kinara cha taa kwa mwanga, vyombo vyake, taa zake na hayo mafuta kwa nuru; 15#Kut 30:1; 37:25; 40:5; 30:23,34; 1 Sam 2:28; 1 Nya 23:13; 2 Nya 29:11; Lk 1:9 na hiyo madhabahu ya kufukizia uvumba, miti yake, hayo mafuta ya kupaka, huo uvumba mzuri na hicho kisitiri cha mlango, mlangoni mwa hiyo maskani; 16#Kut 27:1 na hiyo madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, pamoja na wavu wake wa shaba, miti yake, vyombo vyake vyote hilo birika na kitako chake; 17#Kut 27:9 na hizo kuta za nguo za ua, viguzo vyake, vitako vyake na pazia la lango la ua; 18na vile vigingi vya maskani, vigingi vya ua na kamba zake 19#Kut 31:10; 39:1,41; Hes 4:5,6 na mavazi yenye kufumwa kwa uzuri, kwa ajili ya kutumika ndani ya mahali patakatifu, hayo mavazi matakatifu ya Haruni kuhani, na mavazi ya wanawe, ili kutumika katika kazi ya ukuhani.
Sadaka kwenye hema ya kukutania
20Basi mkutano wote wa wana wa Israeli wakaondoka hapo mbele ya Musa. 21#Kut 25:2; 36:2; 1 Nya 28:2,9; 29:9; Ezr 7:27; 2 Kor 8:12; 9:7 Wakaja kila mtu ambaye moyo wake ulimhimiza, na kila mtu ambaye roho yake ilimfanya kuwa apenda, nao wakaleta sadaka za kumpa BWANA, kwa kazi ya hema ya kukutania, na kwa utumishi wake, na kwa hayo mavazi matakatifu. 22Nao wakaja, wanaume kwa wanawake, wote waliokuwa na moyo wa kupenda, wakaleta vipini, hazama, pete za mhuri, vikuku na vyombo vyote vya dhahabu; kila mtu aliyetoa toleo la dhahabu la kumpa BWANA. 23#1 Nya 29:8 Tena kila mtu aliyeona kwake nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani nzuri, singa za mbuzi, ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu na ngozi za pomboo, akavileta. 24Kila mtu aliyetoa toleo la fedha, na la shaba, akaileta sadaka ya BWANA; na kila mtu, aliyeona kwake mti wa mshita kwa kazi yoyote ya huo utumishi, akauleta. 25#Kut 28:3; 31:6; 36:1; 2 Fal 23:7; Mit 31:19-24 Na wanawake wote waliokuwa na mioyo ya hekima, walisokota kwa mikono yao, nao wakaleta hizo walizokuwa wamezisokota, nguo za rangi ya samawati, na za rangi ya zambarau, na hizo nyuzi nyekundu, na hiyo nguo ya kitani nzuri. 26Na wanawake wote ambao mioyo yao iliwahimiza katika hekima wakasokota hizo singa za mbuzi. 27#1 Nya 29:6; Ezr 2:68 Na hao wakuu wakavileta vile vito vya shohamu, na vito vya kutiwa, kwa hiyo naivera, na kwa hicho kifuko cha kifuani, 28#Kut 30:23 na viungo vya manukato, na mafuta; kwa hiyo taa, na kwa hayo mafuta ya kutiwa, na kwa huo uvumba mzuri. 29#1 Nya 29:9 Wana wa Israeli wakaleta sadaka za kumpa BWANA kwa moyo wa kupenda; wote, wanaume kwa wanawake, ambao mioyo yao iliwafanya kuwa wapenda kuleta kwa hiyo kazi, ambayo BWANA aliamuru ifanywe kwa mkono wa Musa.
Bezaleli na Oholiabu: Mafundi wajenzi
30 # Kut 31:2 Kisha Musa akawaambia wana wa Israeli, Angalieni, BWANA amemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila la Yuda; 31#Mwa 41:38; Ayu 32:8; Mit 2:6 naye amemjaza Roho ya Mungu, katika hekima, na akili, na ujuzi, na kazi ya ustadi kila aina; 32na kuvumbua kazi za werevu, na kufanya kazi ya dhahabu, fedha na shaba, 33na kukata vito vya kutilia, na kuchora miti, atumike katika kazi za ufundi wa kila aina. 34#Kut 31:6 Naye amemtilia moyoni mwake uwezo ili apate kufundisha, yeye, na Oholiabu mwana wa Ahisamaki, wa kabila la Dani. 35#Kut 31:3,6; 36:1,2; 1 Fal 7:14; 2 Nya 2:14; Isa 28:26; Yak 1:5 Amewajaza watu hao ujuzi, ili watumike katika kazi za kila aina, mawe, na kazi ya fundi mwenye kutia taraza, katika nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani nzuri, ya mwenye kufuma nguo; ya hao wafanyao kazi yoyote, na ya wenye kuvumbua kazi za werevu.

Iliyochaguliwa sasa

Kutoka 35: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha