Kutoka 23:16-17
Kutoka 23:16-17 Biblia Habari Njema (BHN)
Mtaadhimisha sikukuu ya mavuno ya kwanza ya kazi zenu na ya mavuno ya mashamba yenu. Mtaadhimisha sikukuu ya kukusanya mavuno mwishoni mwa mwaka mnapokusanya mazao ya kazi zenu. Mara tatu kwa mwaka wanaume wote watakusanyika mbele zangu mimi Bwana Mwenyezi-Mungu.
Kutoka 23:16-17 Swahili Revised Union Version (SRUV)
tena, sikukuu ya mavuno, hayo malimbuko ya kazi zako za kupanda mashambani; tena, sikukuu ya kukusanya, mwisho wa mwaka, hapo utakapokusanya hayo uliyoyataabikia shambani. Mara tatu katika mwaka wana wa kiume wako wote watahudhuria mbele ya Bwana MUNGU.
Kutoka 23:16-17 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
tena, sikukuu ya mavuno, hayo malimbuko ya kazi zako za kupanda mashambani; tena, sikukuu ya kukusanya, mwisho wa mwaka, hapo utakapokusanya hayo uliyoyataabikia shambani. Mara tatu katika mwaka watu waume wako wote watahudhuria mbele ya Bwana MUNGU.
Kutoka 23:16-17 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Utaadhimisha Sikukuu ya Mavuno kwa malimbuko ya mazao yako uliyopanda katika shamba lako. “Utaadhimisha Sikukuu ya Kukusanya mavuno mwishoni mwa mwaka, unapokusanya mavuno yako toka shambani. “Mara tatu kwa mwaka wanaume wote watakuja mbele za BWANA Mwenyezi.