Kutoka 23:1-2
Kutoka 23:1-2 Biblia Habari Njema (BHN)
“Usitoe habari za uongo. Usishirikiane na mtu mwovu ili kuwa shahidi mbaya. Usifuate genge la watu kutenda uovu, wala usijumuike na genge la watu kutoa ushahidi mahakamani ili kupotosha haki.
Kutoka 23:1-2 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Usivumishe habari za uongo; usishirikiane na mwovu kwa kuwa shahidi wa uongo. Usiwafuate walio wengi kutenda uovu; wala usitie ushahidi wako katika neno lolote kwa kugeukia kando na kuandamana na mkutano ili kupotoa hukumu
Kutoka 23:1-2 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Usivumishe habari za uongo; usitie mkono wako pamoja na mwovu, kuwa shahidi wa udhalimu. Usiandamane na mkutano kutenda uovu; wala usitie ushahidi wako katika neno lo lote kwa kugeukia kando na kuandamana na mkutano ili kupotoa hukumu