Waefeso 5:19-20
Waefeso 5:19-20 Biblia Habari Njema (BHN)
Zungumzeni kwa maneno ya Zaburi, nyimbo na tenzi za kiroho; mwimbieni Bwana nyimbo na Zaburi kwa shukrani mioyoni mwenu. Mshukuruni Mungu Baba daima kwa ajili ya yote, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo.
Shirikisha
Soma Waefeso 5Waefeso 5:19-20 Swahili Revised Union Version (SRUV)
mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu; na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo.
Shirikisha
Soma Waefeso 5