Kumbukumbu la Sheria 30:6-7
Kumbukumbu la Sheria 30:6-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atawafanyeni nyinyi na wazawa wenu muwe na moyo wa utii ili mumpende yeye kwa moyo wenu wote na roho yenu yote, mpate kuishi. Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atazifanya laana hizi zote ziwapate adui zenu ambao waliwatesa.
Kumbukumbu la Sheria 30:6-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA, Mungu wako, atautahiri moyo wako, na moyo wa uzao wako, ili umpende BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, upate kuwa hai. Na laana hizi zote BWANA, Mungu wako, atawatia adui zako na hao wakuchukiao, waliokuwa wakikutesa.
Kumbukumbu la Sheria 30:6-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA, Mungu wako, atautahiri moyo wako, na moyo wa uzao wako, ili umpende BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, upate kuwa hai. Na laana hizi zote BWANA, Mungu wako, atawatia adui zako na hao wakuchukiao, waliokuwa wakikutesa.
Kumbukumbu la Sheria 30:6-7 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
BWANA Mungu wako ataitahiri mioyo yenu na mioyo ya wazao wenu ili mweze kumpenda kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote ukaishi. BWANA Mungu wako ataweka laana hizi zote juu ya adui zako ambao wanakuchukia na kukutesa.