Kumbukumbu la Torati 30:6-7
Kumbukumbu la Torati 30:6-7 SRUV
BWANA, Mungu wako, atautahiri moyo wako, na moyo wa uzao wako, ili umpende BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, upate kuwa hai. Na laana hizi zote BWANA, Mungu wako, atawatia adui zako na hao wakuchukiao, waliokuwa wakikutesa.