Kumbukumbu la Sheria 11:8-9
Kumbukumbu la Sheria 11:8-9 Biblia Habari Njema (BHN)
“Tiini amri zote ninazowaamuru siku hii ya leo, ili muweze kuingia na kuimiliki nchi mnayoiendea, mpate kuishi kwa muda mrefu katika nchi hiyo inayotiririka maziwa na asali; nchi ambayo Mwenyezi-Mungu aliahidi kuwapa babu zenu na wazawa wao.
Kumbukumbu la Sheria 11:8-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwa hiyo yaangalieni maagizo yote niwaagizayo leo, mpate kuwa na nguvu, na kuingia mkaimiliki nchi mwivukiayo kuimiliki; nanyi mpate kuzifanya siku zenu kuwa nyingi juu ya nchi BWANA aliyowaapia baba zenu, ya kuwa atawapa wao na kizazi chao, nchi imiminikayo maziwa na asali
Kumbukumbu la Sheria 11:8-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwa hiyo yaangalieni maagizo yote niwaagizayo leo, mpate kuwa na nguvu, na kuingia mkaimiliki nchi mwivukiayo kuimiliki; nanyi mpate kuzifanya siku zenu kuwa nyingi juu ya nchi BWANA aliyowaapia baba zenu, ya kuwa atawapa wao na kizazi chao, nchi imiminikayo maziwa na asali
Kumbukumbu la Sheria 11:8-9 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kwa hiyo fuateni maagizo yote ninayowapa leo, ili mpate kuwa na nguvu za kuingia na kuiteka nchi ile ambayo mnavuka Yordani kuimiliki, ili mpate kuishi siku nyingi katika nchi ile ambayo BWANA aliapa kuwapa baba zenu na wazao wao, nchi itiririkayo maziwa na asali.