Kumbukumbu la Sheria 11:6-7
Kumbukumbu la Sheria 11:6-7 Biblia Habari Njema (BHN)
na mambo aliyowatenda Dathani na Abiramu, wana wa Eliabu, mwana wa Reubeni; jinsi mbele ya watu wote wa Israeli nchi ilivyofunuka na kuwameza pamoja na jamaa zao, mahema yao, wanyama na watumishi wao wote. Maana macho yenu yameona matendo yote haya makubwa ambayo Mwenyezi-Mungu aliyafanya.
Kumbukumbu la Sheria 11:6-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
na alivyowafanya Dathani, na Abiramu, wana wa Eliabu mwana wa Reubeni; nchi ilivyofunua kinywa chake, ikawameza, na walio nyumbani mwao, na mahema yao, na kila kitu kilichokuwa hai kikiwafuata, katikati ya Israeli yote; lakini macho yenu yameiona kazi kubwa ya BWANA aliyoifanya, yote.
Kumbukumbu la Sheria 11:6-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
na alivyowafanya Dathani, na Abiramu, wana wa Eliabu mwana wa Reubeni; nchi ilivyofunua kinywa chake, ikawameza, na walio nyumbani mwao, na mahema yao, na kila kitu kilichokuwa hai kikiwafuata, katikati ya Israeli yote; lakini macho yenu yameiona kazi kubwa ya BWANA aliyoifanya, yote.
Kumbukumbu la Sheria 11:6-7 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
wala lile Mungu alilowafanyia Dathani na Abiramu, wana wa Eliabu wa kabila la Reubeni, wakati ardhi ilipofungua kinywa chake katikati ya Israeli yote, ikawameza pamoja na walio nyumbani mwao, hema zao na kila kitu kilichokuwa hai ambacho kilikuwa mali yao. Bali ilikuwa ni macho yenu wenyewe ambayo yaliyaona mambo haya yote makuu BWANA aliyoyatenda.