Kumbukumbu la Sheria 11:4-5
Kumbukumbu la Sheria 11:4-5 Biblia Habari Njema (BHN)
aliyoyatendea majeshi ya Misri, farasi wao na magari yao ya vita, jinsi alivyozamisha jeshi hilo katika bahari ya Shamu, na jinsi Mwenyezi-Mungu alivyoliangamiza hata hivi leo. Pia kumbukeni aliyowafanyieni Mwenyezi-Mungu jangwani kabla hamjafika hapa
Kumbukumbu la Sheria 11:4-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
na alivyolifanya jeshi la Misri, farasi wao, na magari yao; na alivyowafunika kwa maji ya Bahari ya Shamu walipokuwa wakiwaandama, na alivyowaangamiza BWANA hata hivi leo; na mambo aliyowafanyia ninyi nyikani, hadi mkafika mahali hapa
Kumbukumbu la Sheria 11:4-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
na alivyolifanya jeshi la Misri, farasi zao, na magari yao; na alivyowafunikiza maji ya Bahari ya Shamu walipokuwa wakiwaandamia, na alivyowaangamiza BWANA hata hivi leo; na mambo aliyowafanyia ninyi barani, hata mkaja mahali hapa
Kumbukumbu la Sheria 11:4-5 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
lile alilolifanyia jeshi la Wamisri, farasi na magari yake, jinsi alivyowafurikisha na maji ya Bahari ya Shamu walipokuwa wakiwafuatilia ninyi, na jinsi BWANA alivyowaletea angamizo la kudumu juu yao. Sio watoto wenu walioyaona yale Mungu aliyowafanyia huko jangwani mpaka mkafika mahali hapa