Kumbukumbu la Sheria 11:18-21
Kumbukumbu la Sheria 11:18-21 Biblia Habari Njema (BHN)
“Yawekeni maneno yangu haya mioyoni mwenu na rohoni mwenu. Yafungeni mikononi mwenu kama alama na kuyavaa katika paji la uso. Wafundisheni watoto wenu maneno haya mkiyazungumzia mketipo katika nyumba zenu, mnapotembea, mnapolala na mnapoamka. Ziandikeni katika vizingiti vya nyumba zenu, na katika malango yenu, ili nyinyi na watoto wenu mpate kuishi maisha marefu katika nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, aliapa kuwapa babu zenu, siku zote mbingu zitakapodumu juu ya dunia.
Kumbukumbu la Sheria 11:18-21 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwa hiyo yawekeni maneno yangu mioyoni mwenu na rohoni mwenu; yafungeni yawe dalili juu ya mikono yenu, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yenu. Nayo wafunzeni watoto wenu kwa kuyazungumza uishipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo. Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako; ili siku zenu zifanywe nyingi, na za vijana vyenu nao, juu ya nchi BWANA aliyowaapia baba zenu kuwa atawapa, kama zilivyo siku za mbingu juu ya nchi.
Kumbukumbu la Sheria 11:18-21 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwa hiyo yawekeni maneno yangu mioyoni mwenu na rohoni mwenu; yafungeni yawe dalili juu ya mikono yenu, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yenu. Nayo wafunzeni vijana vyenu kwa kuyazungumza uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo. Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako; ili siku zenu zifanywe nyingi, na za vijana vyenu nao, juu ya nchi BWANA aliyowaapia baba zenu kuwa atawapa, kama zilivyo siku za mbingu juu ya nchi.
Kumbukumbu la Sheria 11:18-21 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Yawekeni haya maneno yangu katika mioyo yenu na akili zenu, yafungeni kama alama juu ya mikono yenu na kwenye paji za nyuso zenu. Wafundisheni watoto wenu, yazungumzeni wakati mketipo nyumbani na wakati mtembeapo njiani, wakati mlalapo na wakati mwamkapo. Yaandikeni juu ya miimo ya nyumba zenu na juu ya malango yenu, ili kwamba siku zenu na siku za watoto wenu zipate kuwa nyingi katika nchi ile BWANA aliyoapa kuwapa baba zenu, kama zilivyo nyingi siku za mbingu juu ya nchi.