Kumbukumbu la Sheria 11:13-15
Kumbukumbu la Sheria 11:13-15 Biblia Habari Njema (BHN)
“Basi, mkizitii amri zangu ninazowapeni leo, mkampenda Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, mkamtumikia kwa moyo wenu wote na kwa roho yenu yote, yeye ataipatia mvua nchi yenu wakati wake, mvua za masika na mvua za vuli, nanyi mtavuna nafaka yenu, divai yenu na mafuta yenu. Ataotesha majani mashambani kwa ajili ya ng'ombe wenu, nanyi mtakula na kushiba.
Kumbukumbu la Sheria 11:13-15 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tena itakuwa, mtakapoyazingatia kwa bidii maagizo yangu niwaagizayo leo, kwa kumpenda BWANA, Mungu wenu, na kumtumikia kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote, ndipo nitakapowapa mvua ya nchi yenu kwa wakati wake, mvua ya masika, na mvua ya vuli, upate kuvuna nafaka yako, na divai yako, na mafuta yako. Nami nitakupa nyasi katika mavue yako kulisha wanyama wako wa mifugo, nawe utakula na kushiba.
Kumbukumbu la Sheria 11:13-15 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tena itakuwa, mtakaposikiza kwa bidii maagizo yangu niwaagizayo leo, kwa kumpenda BWANA, Mungu wenu, na kumtumikia kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote, ndipo nitakapowapa mvua ya nchi yenu kwa wakati wake, mvua ya masika, na mvua ya vuli, upate kuvuna nafaka yako, na divai yako, na mafuta yako. Nami nitakupa nyasi katika mavue yako kulisha wanyama wako wa mifugo, nawe utakula na kushiba.
Kumbukumbu la Sheria 11:13-15 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Hivyo kama mkiyatii maagizo yangu ninayowapa leo kwa uaminifu, yaani kwa kumpenda BWANA Mungu wenu, na kumtumikia kwa moyo wako wote na kwa roho yenu yote, ndipo atawanyweshea mvua katika nchi yenu kwa majira yake, mvua ya masika na ya vuli, ili mpate kuvuna nafaka zenu, divai mpya na mafuta. Nitawapa majani kwa ajili ya ngʼombe wenu, nanyi mtakula na kushiba.