Wakolosai 3:23-25
Wakolosai 3:23-25 Biblia Habari Njema (BHN)
Kila mfanyacho, fanyeni kwa moyo wote, kwa sababu ya Bwana na si kwa ajili ya mtu. Kumbukeni kwamba atawapeni tuzo lile alilowawekea watu wake. Mtumikieni Kristo Bwana! Atendaye mabaya atalipwa kufuatana na ubaya wake; Mungu hana ubaguzi.
Wakolosai 3:23-25 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lolote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu, mkijua ya kuwa mtapokea kwa Bwana ujira wa urithi. Mnamtumikia Bwana Kristo. Maana adhulumuye atapata mapato ya udhalimu wake, wala hakuna upendeleo.
Wakolosai 3:23-25 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu, mkijua ya kuwa mtapokea kwa Bwana ujira wa urithi. Mnamtumikia Bwana Kristo. Maana adhulumuye atapata mapato ya udhalimu wake, wala hakuna upendeleo.
Wakolosai 3:23-25 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Lolote mfanyalo, fanyeni kwa moyo kama watu wanaomtumikia Bwana, na si wanadamu, kwa kuwa mnajua kwamba mtapokea urithi wenu kutoka kwa Bwana ukiwa thawabu yenu. Ni Bwana Yesu Kristo mnayemtumikia. Yeyote atendaye mabaya atalipwa kwa ajili ya mabaya yake, wala hakuna upendeleo.