Matendo 23:33-35
Matendo 23:33-35 Biblia Habari Njema (BHN)
Walipofika Kaisarea walimpa mkuu wa mkoa ile barua na kumweka Paulo chini ya mamlaka yake. Felisi alipoisoma hiyo barua aliwauliza Paulo ametoka mkoa gani. Alipofahamishwa kwamba alikuwa ametoka mkoa wa Kilikia, akasema, “Nitasikiliza kesi yako baada ya washtaki wako kufika.” Kisha akaamuru Paulo awekwe chini ya ulinzi ndani ya ukumbi wa Herode.
Matendo 23:33-35 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na wale walipofika Kaisaria, na kumpa mtawala ile barua, wakamweka Paulo mbele yake. Naye alipokwisha kuisoma, akawauliza, Mtu huyu ni wa mkoa gani? Alipoarifiwa ya kuwa ni mtu wa Kilikia, akasema, Nitakusikia wewe watakapokuja wale waliokushitaki; akaamuru alindwe katika nyumba ya utawala wa Herode.
Matendo 23:33-35 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na wale walipofika Kaisaria, na kumpa liwali ile barua, wakamweka Paulo mbele yake. Naye alipokwisha kuisoma, akawauliza, Mtu huyu ni wa jimbo gani? Alipoarifiwa ya kuwa ni mtu wa Kilikia, akasema, Nitakusikia wewe watakapokuja wale waliokushitaki; akaamuru alindwe katika nyumba ya uliwali ya Herode.
Matendo 23:33-35 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Askari walipofika Kaisaria, walimpa mtawala ile barua, na kumkabidhi Paulo kwake. Mtawala alipokwisha kuisoma ile barua alimuuliza Paulo alikuwa mtu wa jimbo gani. Alipojua kuwa anatoka Kilikia, alisema, “Nitasikiliza shauri lako washtaki wako watakapofika hapa.” Kisha akaamuru Paulo awekwe chini ya ulinzi kwenye jumba la kifalme la Herode.