Matendo 23:23-25
Matendo 23:23-25 Biblia Habari Njema (BHN)
Basi, mkuu wa jeshi aliwaita askari wawili akawaambia, “Wekeni tayari askari 200, wapandafarasi sabini na askari 200 wa mikuki, waende Kaisarea; muwe tayari kuondoka kabla ya saa tatu leo usiku. Wekeni farasi kadhaa kwa ajili ya Paulo; mfikisheni salama kwa Felisi, mkuu wa mkoa.” Halafu mkuu huyo wa jeshi akaandika barua hivi
Matendo 23:23-25 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Akawaita maofisa wawili, akasema, Wekeni tayari askari mia mbili kwenda Kaisaria, na askari wapanda farasi sabini, na wenye mikuki mia mbili, kabla ya saa tatu usiku. Akawaambia kuweka wanyama tayari wampandishe Paulo, na kumchukua salama kwa Feliki mtawala. Akaandika barua, juu ya hili
Matendo 23:23-25 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Akawaita maakida wawili, akasema, Wekeni tayari askari mia mbili kwenda Kaisaria, na askari wapanda farasi sabini, na wenye mikuki mia mbili, kwa saa tatu ya usiku. Akawaambia kuweka wanyama tayari wampandishe Paulo, na kumchukua salama kwa Feliki liwali. Akaandika barua, kwa namna hii
Matendo 23:23-25 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kisha yule jemadari akawaita viongozi wake wawili wa askari akawaambia, “Jiandaeni kuondoka saa tatu usiku huu kuelekea Kaisaria pamoja na askari 200, wapanda farasi sabini na watu 200 wenye mikuki. Pia tayarisheni na farasi watakaotumiwa na Paulo, mkampeleke salama kwa mtawala Feliksi.” Kisha akaandika barua kwa Feliksi kama ifuatavyo