Matendo 2:11-13
Matendo 2:11-13 Biblia Habari Njema (BHN)
Wayahudi na watu walioongokea dini ya Kiyahudi; wengine wametoka Krete na Arabia. Sisi sote tunasikia wakisema kwa lugha zetu wenyewe mambo makuu ya Mungu.” Wote walishangaa na kufadhaika huku wakiulizana, “Hii ina maana gani?” Lakini wengine wakawadhihaki wakisema, “Watu hawa wamelewa divai mpya!”
Matendo 2:11-13 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wakrete na Waarabu; tunawasikia hawa wakisema kwa lugha zetu matendo makuu ya Mungu. Wakashangaa wote wakaingiwa na shaka, wakiambiana, Maana yake nini mambo haya? Wengine walidhihaki, wakisema, wamelewa kwa mvinyo mpya.
Matendo 2:11-13 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wakrete na Waarabu; tunawasikia hawa wakisema kwa lugha zetu matendo makuu ya Mungu. Wakashangaa wote wakaingiwa na shaka, wakiambiana, Maana yake nini mambo haya? Wengine walidhihaki, wakisema, wamelewa kwa mvinyo mpya.
Matendo 2:11-13 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Wayahudi na waongofu, Wakrete na Waarabu, sote tunawasikia watu hawa wakisema mambo makuu ya ajabu ya Mungu katika lugha zetu wenyewe.” Wakiwa wameshangaa na kufadhaika wakaulizana, “Ni nini maana ya mambo haya?” Lakini wengine wakawadhihaki wakasema, “Hawa wamelewa divai!”