1 Samueli 12:6-7
1 Samueli 12:6-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Samueli akawaambia, “Mwenyezi-Mungu ndiye aliyemteua Mose na Aroni na kuwatoa babu zenu nchini Misri. Sasa simameni papo hapo mlipo ili mimi na nyinyi tuhukumiwe mbele ya Mwenyezi-Mungu, nami nitawahutubia kuhusu matendo yake ya ajabu ambayo aliyatenda ili kuwaokoa nyinyi na babu zenu.
1 Samueli 12:6-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Samweli akawaambia watu, Ni yeye BWANA aliyewaweka Musa na Haruni, yeye ndiye aliyewatoa baba zenu kutoka nchi ya Misri. Basi sasa simameni, ili niwahutubie mbele za BWANA, kwa kutaja matendo yote ya haki ya BWANA, aliyowatendea ninyi na baba zenu.
1 Samueli 12:6-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Samweli akawaambia watu, Ni yeye BWANA aliyewaweka Musa na Haruni, ndiye yeye aliyewatoa baba zenu kutoka nchi ya Misri. Basi sasa simameni, ili niwahutubie mbele za BWANA, kwa kutaja matendo yote ya haki ya BWANA, aliyowatendea ninyi na baba zenu.
1 Samueli 12:6-7 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kisha Samweli akawaambia watu, “BWANA ndiye alimchagua Mose na Aroni, na kuwaleta baba zenu akiwapandisha kutoka Misri. Sasa basi, simameni hapa, kwa sababu nitakabiliana nanyi kwa ushahidi mbele za BWANA wa matendo yote ya haki yaliyofanywa na BWANA kwenu na kwa baba zenu.