1 Samueli 12:22-23
1 Samueli 12:22-23 Biblia Habari Njema (BHN)
Kwa heshima ya jina lake kuu, Mwenyezi-Mungu hatawatupa watu wake kwa sababu amependa kuwafanya nyinyi muwe watu wake. Tena kwa upande wangu haitatokea niache kuwaombea kwa Mwenyezi-Mungu; kufanya hivyo itakuwa kumkosea Mwenyezi-Mungu. Nitaendelea kuwafundisha njia njema na ya haki.
1 Samueli 12:22-23 Swahili Revised Union Version (SRUV)
visivyoweza kusaidia wala kuokoa, kwa kuwa havifai kitu. Maana BWANA hatawaacha watu wake kwa ajili ya jina lake kuu; kwa kuwa imempendeza BWANA kuwafanya ninyi kuwa watu wake mwenyewe. Lakini mimi, hasha! Nisimtende BWANA dhambi kwa kuacha kuwaombea ninyi; lakini nitawaelimisha katika njia iliyo njema, na kunyoka
1 Samueli 12:22-23 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
visivyoweza kusaidia wala kuokoa, kwa kuwa havifai kitu. Maana BWANA hatawaacha watu wake kwa ajili ya jina lake kuu; kwa kuwa imempendeza BWANA kuwafanya ninyi kuwa watu wake mwenyewe. Walakini mimi, hasha! Nisimtende BWANA dhambi kwa kuacha kuwaombea ninyi; lakini nitawaelimisha katika njia iliyo njema, na kunyoka
1 Samueli 12:22-23 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kwa ajili ya jina lake kuu BWANA hatawakataa watu wake, kwa sababu ilimpendeza BWANA kuwafanya kuwa wake mwenyewe. Kwa habari yangu, iwe mbali nami kutenda dhambi dhidi ya BWANA kwa kushindwa kuwaombea. Mimi nitawafundisha njia iliyo njema na ya kunyooka.