1 Samueli 12:18-19
1 Samueli 12:18-19 Biblia Habari Njema (BHN)
Basi, Samueli akamwomba Mwenyezi-Mungu, naye akatuma radi na mvua katika siku hiyo. Watu wote wakamwogopa sana Mwenyezi-Mungu na Samueli. Hivyo wakamwambia Samueli, “Tafadhali utuombee sisi watumishi wako kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ili tusife; kwa sababu tumezidisha dhambi zetu kwa uovu huo wa kujitakia mfalme.”
1 Samueli 12:18-19 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi Samweli akamwomba BWANA, naye BWANA akatuma ngurumo na mvua siku ile; nao watu wote wakamwogopa BWANA sana, na Samweli pia. Watu wote wakamwambia Samweli, Tuombee watumishi wako kwa BWANA, Mungu wako, tusije tukafa; maana tumeongeza dhambi zetu zote kwa uovu huu, wa kujitakia mfalme.
1 Samueli 12:18-19 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi Samweli akamwomba BWANA, naye BWANA akapeleka ngurumo na mvua siku ile; nao watu wote wakamwogopa BWANA sana, na Samweli pia. Watu wote wakamwambia Samweli, Utuombee sisi watumwa wako kwa BWANA, Mungu wako, tusije tukafa; maana tumeongeza dhambi zetu zote kwa uovu huu, wa kujitakia mfalme.
1 Samueli 12:18-19 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kisha Samweli akamwomba BWANA, na siku ile ile BWANA akatuma ngurumo na mvua. Hivyo watu wote wakamwogopa sana BWANA na Samweli. Watu wote wakamwambia Samweli, “Mwombe BWANA Mungu wako kwa ajili ya watumishi wako, ili tusije tukafa, kwa kuwa tumeongeza uovu juu ya dhambi zetu nyingine kwa kuomba mfalme.”