1 Samueli 12:16-17
1 Samueli 12:16-17 Biblia Habari Njema (BHN)
Kwa hiyo basi, tulieni na kulitazama jambo hilo kubwa ambalo Mwenyezi-Mungu atatenda mbele yenu. Je, sasa si wakati wa kuvuna ngano? Lakini mimi nitamwomba Mwenyezi-Mungu alete radi na mvua, nanyi mtatambua na kuona kuwa uovu wenu mliotenda mbele ya Mwenyezi-Mungu kwa kujitakia mfalme, ni mkubwa.”
1 Samueli 12:16-17 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na sasa simameni, mkalione jambo hili kubwa, BWANA atakalolitenda mbele ya macho yenu. Je! Leo si mavuno ya ngano? Nitamwomba BWANA, kwamba atume ngurumo na mvua; nanyi mtajua na kuona ya kuwa uovu wenu mlioufanya machoni pa BWANA, ni mwingi sana, kwa kujitakia mfalme.
1 Samueli 12:16-17 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na sasa simameni, mkalione jambo hili kubwa, BWANA atakalolitenda mbele ya macho yenu. Leo je! Si mavuno ya ngano? Nitamwomba BWANA, kwamba apeleke ngurumo na mvua; nanyi mtajua na kuona ya kuwa uovu wenu ni mwingi sana, mlioufanya machoni pa BWANA, kwa kujitakia mfalme.
1 Samueli 12:16-17 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Sasa basi, simameni kimya mkaone jambo hili kubwa ambalo BWANA anakwenda kulifanya mbele ya macho yenu! Je, sasa si mavuno ya ngano? Nitamwomba BWANA ili alete ngurumo na mvua. Nanyi mtatambua jambo hili lilivyo baya mlilolifanya mbele za macho ya BWANA mlipoomba mfalme.”