1 Petro 4:5-6
1 Petro 4:5-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini watapaswa kutoa hoja juu ya jambo hilo mbele yake Mungu aliye tayari kuwahukumu walio hai na waliokufa! Ndiyo maana Habari Njema ilihubiriwa hata kwa hao waliokufa, ili baada ya kuhukumiwa katika maisha yao ya kimwili kama wengine, waishi kwa ajili ya Mungu kwa njia ya Roho.
1 Petro 4:5-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nao watatoa hesabu kwake yeye aliye tayari kuwahukumu walio hai na waliokufa. Maana kwa ajili hiyo hata hao waliokufa walihubiriwa Injili, ili kwamba wahukumiwe katika mwili kama wahukumiwavyo wanadamu; bali wawe hai katika roho kama Mungu alivyo hai.
1 Petro 4:5-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nao watatoa hesabu kwake yeye aliye tayari kuwahukumu walio hai na waliokufa. Maana kwa ajili hiyo hata hao waliokufa walihubiriwa Injili, ili kwamba wahukumiwe katika mwili kama wahukumiwavyo wanadamu; bali wawe hai katika roho kama Mungu alivyo hai.
1 Petro 4:5-6 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Lakini itawapasa wao kutoa hesabu mbele zake yeye aliye tayari kuwahukumu walio hai na waliokufa. Kwa kuwa hii ndiyo sababu Injili ilihubiriwa hata kwa wale waliokufa, ili wahukumiwe sawasawa na wanadamu wengine katika mwili, lakini katika roho waishi kulingana na Mungu aishivyo.