Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Petro 4

4
Mawakili wema na neema ya Mungu
1 # Rum 6:2,7 Basi kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake, ninyi nanyi jivikeni silaha ya nia ile ile; kwa maana yeye aliyeteswa katika mwili ameachana na dhambi. 2#1 Yoh 2:16,17 Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani. 3#Efe 2:2,3; Tit 3:3 Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuishi katika uzinzi, tamaa, ulevi, na karamu za kula na kunywa vileo kupindukia, na ibada haramu ya sanamu; 4mambo ambayo wao huona kuwa ni ajabu ya ninyi kutokwenda mbio pamoja nao katika ufisadi ule ule usio na kiasi, wakiwatukana. 5#Mdo 10:42; 2 Tim 4:1; Rum 14:9,10 Nao watatoa hesabu kwake yeye aliye tayari kuwahukumu walio hai na waliokufa. 6#1 Pet 3:19; Rum 8:10; 1 Kor 5:5 Maana kwa ajili hiyo hata hao waliokufa walihubiriwa Injili, ili kwamba wahukumiwe katika mwili kama wahukumiwavyo wanadamu; bali wawe hai katika roho kama Mungu alivyo hai.
7 # 1 Kor 10:11; 1 Yoh 2:18 Lakini mwisho wa mambo yote umekaribia; basi, iweni na akili, mkeshe katika sala. 8#Mit 10:12; 1 Pet 1:22; Yak 5:20; 1 Kor 13:7 Zaidi ya yote iweni na bidii kubwa katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi. 9#Ebr 13:2 Mkaribishane ninyi kwa ninyi, pasipo kunung'unika; 10#Lk 12:42 kila mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu. 11#Rum 3:2; 12:7; 1 Kor 10:31 Mtu akisema, na aseme kama asemaye maneno halisi ya Mungu; mtu akihudumu, na ahudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu; ili Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo. Utukufu na uweza una yeye hata milele na milele. Amina.
Kuteseka kama Mkristo
12 # 1 Pet 1:6,7 Wapenzi, msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho. 13#Mdo 5:41; Yak 1:2; Rum 8:17; 2 Tim 2:12 Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili pia katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe. 14#1 Pet 2:20; Isa 11:2; Zab 89:50,51 Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni heri yenu; kwa kuwa Roho wa utukufu na wa Mungu anawakalia. 15Lakini pasiwe na hata mmoja wenu atakayeteseka kwa kuwa mwuaji, mwizi, mhalifu au hata mfitini. 16#Mdo 11:26; Flp 1:20 Lakini ikiwa mtu yeyote miongoni mwenu anateseka kwa sababu ni Mkristo, asione haya, bali amtukuze Mungu maana ana jina hili. 17#Eze 9:6; Yer 25:29; 2 The 1:8 Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika nyumba ya Mungu; na ikianza kwetu sisi, mwisho wao wasioitii Injili ya Mungu utakuwaje? 18#Mit 11:31; Lk 23:31 Na mwenye haki akiokoka kwa shida, yule asiyemcha Mungu na mwenye dhambi ataonekana wapi? 19#Zab 31:5 Basi wao wateswao kwa mapenzi ya Mungu na wamwekee amana roho zao, katika kutenda mema, kama kwa Muumba mwaminifu.

Iliyochaguliwa sasa

1 Petro 4: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha