1 Wafalme 6:17-18
1 Wafalme 6:17-18 Biblia Habari Njema (BHN)
Nyumba ile iliyokuwa mbele ya mahali patakatifu sana, ilikuwa na urefu wa mita 18. Mbao za mierezi zilizotanda ukuta wa nyumba kwa ndani zilikuwa zimepambwa kwa michoro ya mibuyu na maua yaliyochanua. Kila sehemu ilikuwa imefunikwa kwa mbao za mierezi, wala hapana jiwe lililoonekana.
1 Wafalme 6:17-18 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nayo nyumba, ndiyo hekalu la mbele, ilikuwa mikono arubaini. Na ndani ya nyumba, mlikuwa na mwerezi ulionakishiwa maboga na maua yaliyofunuka wazi; mlikuwa na mwerezi mahali pote; wala mawe hayakuonekana.
1 Wafalme 6:17-18 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nayo nyumba, ndiyo hekalu la mbele, ilikuwa mikono arobaini. Na ndani ya nyumba, mlikuwa na mwerezi ulionakishiwa maboga na maua yaliyofunuka wazi; mlikuwa na mwerezi mahali pote; wala mawe hayakuonekana.
1 Wafalme 6:17-18 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ukumbi mkubwa uliokuwa mbele ya chumba hiki ndio ulikuwa na urefu wa dhiraa arobaini. Hekalu ndani ilikuwa ya mierezi iliyonakshiwa mifano ya maboga na maua yaliyochanua. Kila kitu kilikuwa cha mwerezi, hakuna jiwe ambalo lilionekana.