1 Mambo ya Nyakati 24:6
1 Mambo ya Nyakati 24:6 Biblia Habari Njema (BHN)
Naye Shemaya mwana wa Nathaneli, mwandishi, aliyekuwa Mlawi, aliwaandika mbele ya mfalme Daudi, maofisa wake, kuhani Sadoki, Ahimeleki mwana wa Abiathari na viongozi wa jamaa za makuhani na za Walawi. Ukoo wa Eleazari ulipata kura mbili, na ukoo wa Ithamari kura moja.
1 Mambo ya Nyakati 24:6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Naye Shemaya, mwana wa Nethaneli, mwandishi, aliyekuwa wa Walawi, akawaandika mbele ya mfalme, na mbele ya wakuu, na Sadoki kuhani, na Ahimeleki, mwana wa Abiathari, na wakuu wa koo za baba za makuhani, na za Walawi; ikatwaliwa ya Eleazari koo moja ya baba, na moja ikatwaliwa ya Ithamari.
1 Mambo ya Nyakati 24:6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Naye Shemaya, mwana wa Nethaneli, mwandishi, aliyekuwa wa Walawi, akawaandika mbele ya mfalme, na mbele ya wakuu, na Sadoki kuhani, na Ahimeleki, mwana wa Abiathari, na wakuu wa mbari za baba za makuhani, na za Walawi; ikatwaliwa ya Eleazari mbari moja ya baba, na moja ikatwaliwa ya Ithamari.
1 Mambo ya Nyakati 24:6 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Mwandishi Shemaya mwana wa Nethaneli, Mlawi, aliorodhesha majina yao mbele ya Mfalme Daudi na maafisa: Kuhani Sadoki, Ahimeleki mwana wa Abiathari, na viongozi wa jamaa za makuhani na za Walawi: jamaa moja ikitoka upande wa Eleazari na nyingine upande wa Ithamari.