1 Mambo ya Nyakati 24:1-2
1 Mambo ya Nyakati 24:1-2 Biblia Habari Njema (BHN)
Hayo ndiyo makundi ya wazawa wa Aroni. Aroni alikuwa na wana wanne: Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari. Nadabu na Abihu walikufa kabla ya baba yao, wala hawakuwa na watoto; kwa hiyo ndugu zao Eleazari na Ithamari wakawa makuhani.
1 Mambo ya Nyakati 24:1-2 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na zamu za wana wa Haruni ni hizi. Wana wa Haruni; Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari. Lakini hao Nadabu na Abihu walikufa kabla ya baba yao, wala hawakuwa na watoto; kwa hiyo Eleazari na Ithamari wakafanya ukuhani.
1 Mambo ya Nyakati 24:1-2 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na zamu za wana wa Haruni ni hizi. Wana wa Haruni; Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari. Lakini hao Nadabu na Abihu walikufa kabla ya baba yao, wala hawakuwa na watoto; kwa hiyo Eleazari na Ithamari wakafanya ukuhani.
1 Mambo ya Nyakati 24:1-2 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Hii ndiyo migawanyo ya wana wa Aroni: Aroni alikuwa na wana wanne: Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari. Nadabu na Abihu walikufa kabla ya baba yao, nao hawakuwa na wana; kwa hiyo ndugu zao Eleazari na Ithamari wakahudumu kama makuhani.