Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 76

76
Mungu mshindi
(Kwa Mwimbishaji: Na ala za nyuzi za muziki. Zaburi ya Asafu. Wimbo)
1Mungu anajulikana katika Yuda;
jina lake ni kuu katika Israeli.
2Makao yake yamo huko Salemu;#76:2 Salemu: Jina la zamani la Yerusalemu.
maskani yake huko Siyoni.
3Huko alivunja mishale ya adui;
alivunja ngao, panga na silaha za vita.
4Wewe, ee Mungu, watukuka mno;
umejaa fahari kuliko milima ya milele.#76:4 milima ya milele: Kulingana na tafsiri ya Kigiriki. Kiebrania ni: Milima ya mawindo.
5Wenye nguvu walipokonywa nyara zao,
sasa wamelala usingizi wa kifo,
mashujaa wa vita hawakuweza kutumia mikono yao.
6Ulipowakemea, ee Mungu wa Yakobo,
farasi na wapandafarasi walikufa ganzi.
7Wewe, ee Mungu, ni wa kutisha mno!
Nani awezaye kustahimili mbele yako ukikasirika?
8Ulijulisha hukumu yako toka mbinguni;
dunia iliogopa na kunyamaza;
9wakati ulipoinuka kutekeleza hukumu,
kuwaokoa wote wanaodhulumiwa duniani.
10Ghadhabu ya watu husababisha tu sifa kwako;
na waliookoka vitani watafanya sikukuu zako.#76:10 watafanya sikukuu zao: Makala moja ya kale; maana katika Kiebrania si dhahiri.
11Mtimizieni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu ahadi zenu;
enyi mlio karibu mpeni zawadi Mungu wa kutisha.
12Yeye huzitoa roho za wakuu;
huwatisha wafalme wa dunia.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 76: BHN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha