Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Wafilipi 1

1
Salamu
1 # Mdo 16:12; 1 Kor 1:2; 1 Tim 3:1,8 Paulo na Timotheo, watumwa wa Kristo Yesu, kwa watakatifu wote katika Kristo Yesu, walioko Filipi, pamoja na maaskofu#1:1 Askofu: maana yake ni, Mwangalizi. na mashemasi.#1:1 Shemasi: maana yake ni, Mtumishi wa kanisa. 2#Rum 1:7 Neema na iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.
Ombi la Paulo kwa Wafilipi
3 # Rum 1:8; 1 Kor 1:4 Namshukuru Mungu wangu kila niwakumbukapo, 4sikuzote kila niwaombeapo ninyi nyote nikisema sala zangu kwa furaha, 5kwa sababu ya ushirika wenu katika kuieneza Injili, tangu siku ile ya kwanza hata hivi leo. 6#Flp 2:13; 1 Kor 1:6-8 Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu; 7vile vile kama ilivyo wajibu wangu kufikiri haya juu yenu nyote; kwa sababu ninyi mmo moyoni mwangu; kwa kuwa katika kufungwa kwangu na katika kazi ya kutetea Injili na kuithibitisha, ninyi nyote mmeshirikiana nami neema hii. 8#Rum 1:9; 2 Kor 1:23; 1 The 2:5 Maana Mungu ni shahidi wangu, jinsi ninavyowaonea shauku ninyi nyote katika moyo wake Kristo Yesu. 9Na hii ndiyo dua yangu, kwamba pendo lenu lizidi kuwa jingi sana, katika hekima na ufahamu wote; 10#Rum 2:18; 12:2; 1 The 5:23; Ebr 5:14 mpate kuyakubali yaliyo mema; ili mpate kuwa na mioyo safi, bila kosa, mpaka siku ya Kristo; 11#Efe 5:9; 1:6,12,14; Yn 15:8 akiwa mmejazwa matunda ya haki, kwa njia ya Yesu Kristo, kwa utukufu na sifa ya Mungu.
Hali ya sasa ya Paulo
12 # 2 Tim 2:9 Lakini, ndugu zangu, nataka mjue ya kuwa mambo yote yaliyonipata yametokea zaidi kwa kuieneza Injili; 13#Mdo 28:30; Flp 4:22; Efe 3:1 hata vifungo vyangu vimekuwa dhahiri katika Kristo, miongoni mwa askari, na kwa wengine wote pia. 14Na wengi wa hao ndugu walio katika Bwana, wakapata kuthibitika kwa ajili ya kufungwa kwangu, wamezidi sana kuthubutu kunena neno la Mungu pasipo hofu. 15Wengine wanahubiri habari za Kristo kwa sababu ya husuda na fitina; na wengine kwa nia njema. 16Hawa wanamhubiri kwa pendo, wakijua ya kuwa nimewekwa ili niitetee Injili; 17bali wengine wanamhubiri Kristo kwa fitina, wala si kwa moyo mweupe, wakidhani kuongeza dhiki za kufungwa kwangu. 18#Flp 2:17,18 Yadhuru nini? Lakini kwa njia zote, ikiwa ni kwa hila, au ikiwa ni kwa kweli, Kristo anahubiriwa; na kwa hiyo nafurahi, naam, nami nitafurahi. 19#Ayu 13:16; 2 Kor 1:11 Maana najua ya kuwa haya yatanigeukia kuwa wokovu wangu, kwa sababu ya kuomba kwenu, na kuruzukiwa Roho wa Yesu Kristo; 20#1 Pet 4:16 kama vile nilivyotazamia sana, na kutumaini, kwamba sitaaibika kamwe, bali kwa uthabiti wote, kama sikuzote na sasa vivyo hivyo Kristo ataadhimishwa katika mwili wangu; ikiwa kwa maisha yangu, au ikiwa kwa mauti yangu. 21#Gal 2:20 Kwa maana kwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni faida. 22#Rum 1:13 Ila ikiwa kuishi katika mwili, kwangu mimi ni matunda ya kazi; basi nitakalolichagua silitambui. 23#1 Fal 19:4; 2 Kor 5:8 Ninasongwa katikati ya mambo mawili; ninatamani kwenda zangu nikae na Kristo maana ni vizuri zaidi sana; 24bali kudumu katika mwili kwahitajiwa zaidi kwa ajili yenu. 25Nami nikitumaini hayo, najua ya kuwa nitakaa na kudumu pamoja nanyi, ili mpate kuendelea na kufurahi katika imani; 26hata mzidi kuona fahari katika Kristo Yesu juu yangu kwa sababu ya kuwapo kwangu pamoja nanyi tena.
27 # Kol 1:10; Flp 4:3; 1 The 2:12 Lakini mwenendo wenu na uwe kama inavyoipasa Injili ya Kristo, ili, nikija na kuwaona ninyi, au nisipokuwapo, niyasikie mambo yenu, kama mnasimama imara katika roho moja, kwa moyo mmoja mkiishindania imani ya Injili; 28wala hamwaogopi adui zenu, katika neno lolote; kwao hao ni ishara thabiti ya kuangamizwa, bali kwenu ninyi ni ishara ya wokovu, huo utokao kwa Mungu. 29Maana mmepewa kwa ajili ya Kristo, si kumwamini tu, ila na kuteswa kwa ajili yake; 30#Mdo 16:19-40 mkiwa na mashindano yale yale mliyoyaona kwangu, na kusikia kwamba ninayo hata sasa.

Iliyochaguliwa sasa

Wafilipi 1: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha