Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Marko 1

1
Mahubiri ya Yohana Mbatizaji
1Mwanzo wa Injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu. 2#Mal 3:1; Mt 11:10; Yn 3:28 Kama ilivyoandikwa katika nabii Isaya,
Tazama, namtuma mjumbe wangu
Mbele ya uso wako,
Atakayeitengeneza njia yako.#Mt 3:1-12; Lk 3:1-18; Yn 1:19-30
3 # Isa 40:3 Sauti ya mtu aliaye nyikani,
Itengenezeni njia ya Bwana,
Yanyosheni mapito yake.
4Yohana alitokea, akibatiza nyikani, na kuuhubiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi. 5Wakamwendea nchi yote ya Yudea, nao wa Yerusalemu wote, wakabatizwa katika mto wa Yordani, wakiziungama dhambi zao. 6#2 Fal 1:8; Zek 13:4 Na Yohana alikuwa amevaa singa za ngamia na mshipi wa ngozi kiunoni mwake, akala nzige na asali ya mwituni. 7#Mdo 13:25 Akahubiri akisema, Yuaja nyuma yangu aliye na nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuinama na kuilegeza gidamu ya viatu vyake. 8Mimi niliwabatiza kwa maji; bali yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu.
Kubatizwa kwa Yesu
9 # Lk 2:51 Ikawa siku zile, Yesu alikuja kutoka Nazareti ya Galilaya, akabatizwa na Yohana katika Yordani.#Mt 3:13-17; Lk 3:21-22; Yn 1:31-34 10Mara alipopanda kutoka majini, akaona mbingu zinapasuka, na Roho, kama hua, akishuka juu yake; 11#Mwa 22:2; Zab 2:7; Isa 42:1; Mt 3:17; 12:18; Mk 9:7; Lk 3:22 na sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu; nimependezwa nawe.
Kujaribiwa kwa Yesu
12 # Mt 4:1-11; Lk 4:1-13 Mara Roho akamtoa aende nyikani. 13#Zab 91:13; Yn 1:51 Akawako huko jangwani siku arubaini, hali akijaribiwa na Shetani; naye alikuwa pamoja na wanyama wa mwituni, na malaika walikuwa wakimhudumia.
Mwanzo wa huduma katika Galilaya
14 # Mt 4:12-17; Lk 4:14,15 Hata baada ya Yohana kutiwa gerezani, Yesu akaenda Galilaya, akiihubiri Habari Njema ya Mungu, 15#Mt 3:2; Gal 4:4 akisema, Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili.
Yesu awaita wanafunzi wa kwanza
16 # Mt 4:18-22; Lk 5:1-11 Naye alipokuwa akipita kando ya bahari ya Galilaya, akamwona Simoni na Andrea nduguye, wakitupa jarife baharini; kwa maana walikuwa wavuvi. 17#Mt 13:47 Yesu akawaambia, Njooni mnifuate, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu. 18Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata.
19Akaendelea mbele kidogo, akamwona Yakobo wa Zebedayo, na Yohana nduguye, nao pia walikuwa katika mashua, wakizitengeneza nyavu zao. 20Mara akawaita, wakamwacha baba yao Zebedayo ndani ya mashua pamoja na wafanya kazi wakaenda, wakamfuata.
Mtu mwenye pepo mchafu
21 # Lk 4:31-37 Wakashika njia mpaka Kapernaumu, na mara siku ya sabato akaingia katika sinagogi, akafundisha.#Mt 4:13 22#Mt 7:28,29 Wakashangaa mno kwa mafundisho yake; kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye mamlaka, wala si kama waandishi. 23Na mara palikuwapo ndani ya sinagogi lao mtu mwenye pepo mchafu; akapaza sauti, 24#Mk 5:7; Zab 16:10 akisema, Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Je! Umekuja kutuangamiza? 25Nakutambua u nani, Mtakatifu wa Mungu. Yesu akamkemea, akisema, Fumba kinywa, umtoke. 26#Mk 9:26 Yule pepo mchafu akamtia kifafa, akalia kwa sauti kuu, akamtoka. 27Wakashangaa wote, hata wakaulizana, wakisema, Nini hii? Ni elimu mpya! Maana kwa uweza awaamuru hata pepo wachafu, nao wamtii! 28Habari zake zikaenea haraka kote katika nchi zote kandokando ya Galilaya.
Yesu awaponya wengi katika nyumba ya Simoni
29 # Mt 8:14-16; Lk 4:38-41 Na mara walipotoka katika sinagogi, walifika nyumbani kwa Simoni na Andrea, pamoja na Yakobo na Yohana. 30Naye mkwewe Simoni, mamaye mkewe, alikuwa kitandani, akiugua homa; na mara wakamwambia habari zake. 31Akamkaribia, akamwinua kwa kumshika mkono, homa ikamwacha, akaanza kuwatumikia.
32Hata kulipokuwa jioni, na jua limekwisha kuchwa, walikuwa wakimletea wote waliokuwa wagonjwa, na wenye pepo. 33Na mji wote ulikuwa umekusanyika mlangoni. 34#Lk 4:41; Mdo 16:17,18 Akaponya wengi waliokuwa na maradhi mbalimbali, akatoa pepo wengi, wala hakuwaacha pepo kunena, kwa sababu walimjua.
Yesu ahubiri katika Galilaya
35 # Lk 4:42-44 Hata alfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko. 36Simoni na wenziwe wakamfuata; 37nao walipomwona wakamwambia, Watu wote wanakutafuta. 38Akawaambia, Twendeni mahali pengine, katika vijiji vilivyo karibu, nipate kuhubiri huko nako; maana nilikuja kwa ajili ya hilo. 39#Mt 4:23; 9:35 Akaenda akihubiri katika masinagogi yao, katika nchi yote ya Galilaya, na kutoa pepo.
Yesu amtakasa mtu mwenye ukoma
40 # Mt 8:2-4; Lk 5:12-16 Akaja kwake mtu mwenye ukoma, akamsihi na kumpigia magoti, na kumwambia, Ukitaka, waweza kunitakasa. 41Naye akamhurumia, akanyosha mkono wake, akamgusa, akamwambia, Nataka, takasika. 42Na mara ukoma wake ukamtoka, akatakasika. 43#Mk 3:12; 7:36 Akamkataza kwa nguvu, akamwondoa mara, 44#Law 14:1-32; Law 13:49 akamwambia, Angalia, usimwambie mtu neno lolote, ila nenda zako ukajioneshe kwa kuhani, ukatoe alivyoamuru Musa kwa ajili ya kutakasika kwako, iwe ushuhuda kwao. 45Lakini akatoka, akaanza kuhubiri maneno mengi, na kulitangaza lile neno, hata Yesu asiweze tena kuingia mjini waziwazi; bali alikaa nje mahali pasipokuwa na watu, wakamwendea kutoka kila upande.

Iliyochaguliwa sasa

Marko 1: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha