Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mika UTANGULIZI

UTANGULIZI
Neno “Mika” katika lugha ya Kiebrania ni kifupisho cha jina “Mikaya”, maana yake “ni nani aliye kama BWANA?” Nabii Mika aliyetoa ujumbe wa kitabu hiki ni mtu tofauti na nabii aliye na jina linalofanana na hilo, yaani Mikaya (1 Fal 26:18, Mik 1:1,14). Mika alikuwa mkulima na mfugaji. Alitoa ujumbe nyakati zile zile za nabii Isaya katikati ya karne ya nane Kabla ya Kristo Kuzaliwa kwa wakazi wa Ufalme wa Kusini uitwao Yuda (tazama Isa 1:1). Kwa kuwa ujumbe wa Mika sehemu nyingi unashabihiana na ujumbe wa Isaya, wataalamu wa mambo ya Biblia wanahisi kwamba huenda Mika alikuwa mwanafunzi mmojawapo wa Isaya (Isa 8:16).
Katikati ya karne ya nane Kabla ya Kristo ukulima na biashara vilistawi katika Israeli na Yuda. Hata hivyo maovu nayo yalishamiri pia (tazama tangulizi za Isaya, Hosea na Amosi). Viongozi wa dini walihubiri maneno ya kuunga mkono dhuluma na udhalimu ili wapate riziki yao hata kumlaumu nabii Mika kuhusiana na ujumbe alioutoa (2:6,11 na 3:5). Mika kama manabii wengine wa BWANA wa wakati huo alikemea hali hiyo.
Ujumbe uliotolewa na Mika ni jumlisho la unabii wa manabii wote wa nyakati hizo. Mungu anataka watu wake wageuze nia na matendo yao, watende yote kwa haki, wapende kuwa na huruma na kuishi kwa unyenyekevu mbele za Mungu wao (6:8). Mika anawaonya watu kuwa wasipotubu miji yao mikuu itabomolewa na falme zao zitaangamizwa. Mika alitabiri hali mpya ya wokovu. Watu watakaobaki wataokoka na mfalme wa amani atazaliwa huko Bethlehemu Efrata ambaye atatunza kundi kufuata mapenzi ya BWANA (2:12-13; 4:1-4; 5:2,4) na aibu yao itabadilishwa kuwa utukufu (5:1).
Yaliyomo:
1. Hukumu ya Mungu juu ya Israeli na Yuda, Sura 1—3
2 Ahadi ya Mungu ya kuhusu utawala wa Masihi, Sura 4—5
3. Kesi mpya ya Israeli, Sura 6:1—7:7
4. Toba na matumaini, Sura 7:8-20

Iliyochaguliwa sasa

Mika UTANGULIZI: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha