Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Luka 17

17
Baadhi ya maneno ya Yesu
1Akawaambia wanafunzi wake, Vikwazo havina budi kuja, lakini ole wake mtu yule ambaye vinakuja kwa sababu yake! 2#Mt 18:6,7 Ingemfaa zaidi mtu huyo jiwe la kusagia lifungwe shingoni mwake, akatupwe baharini, kuliko kumkosesha mmojawapo wa wadogo hawa. 3#Mt 18:15 Jilindeni; kama ndugu yako akikosa, mwonye; akitubu msamehe. 4#Mt 18:21,22 Na kama akikukosea mara saba katika siku moja, na kurudi kwako mara saba, akisema, Nimetubu, msamehe.
5 # Mk 9:24 Mitume wakamwambia Bwana, Tuongezee imani. 6#Mt 17:20; 21:21 Bwana akasema, Kama mngekuwa na imani kiasi cha chembe ya haradali, mngeuambia mkuyu huu, Ng'oka, ukapandwe baharini, nao ungewatii. 7Lakini, ni nani kwenu mwenye mtumwa alimaye au achungaye ng'ombe, atakayemwambia mara arudipo kutoka shambani, Njoo upesi, keti, ule chakula? 8Je! Hatamwambia, Nitayarishie chakula, nile; jifunge unitumikie, hata niishe kula na kunywa, ndipo nawe utakapokula na kunywa? 9Je! Atampa asante yule mtumwa, kwa sababu ameyafanya aliyoagizwa? 10Vivyo hivyo nanyi, mtakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; tumefanya tu yaliyotupasa kufanya.
Yesu awaponya watu kumi wenye ukoma
11 # Lk 9:51; 13:22 Ikawa walipokuwa njiani kwenda Yerusalemu, alikuwa akipita katikati ya Samaria na Galilaya. 12#Law 13:45,46 Na alipoingia katika kijiji kimoja, alikutana na watu kumi wenye ukoma; wakasimama mbali, 13wakapaza sauti wakisema, Ee Yesu, Bwana mkubwa, uturehemu! 14#Law 13:49; 14:1-32; Lk 5:14 Alipowaona aliwaambia, Nendeni, mkajioneshe kwa makuhani. Ikawa walipokuwa wakienda walitakasika. 15Na mmoja wao alipoona kwamba amepona, alirudi, huku akimtukuza Mungu kwa sauti kuu; 16akaanguka kifudifudi miguuni pake, akamshukuru; naye alikuwa Msamaria. 17Yesu akajibu, akanena, Hawakutakaswa wote kumi? Wale tisa wako wapi? 18Je! Hawakuonekana waliorudi kumpa Mungu utukufu ila mgeni huyu? 19#Lk 7:50 Akamwambia, Inuka, nenda zako, imani yako imekuokoa.
Kuja kwa ufalme
20 # Yn 18:36; 3:3 Na alipoulizwa na Mafarisayo, Ufalme wa Mungu utakuja lini? Aliwajibu akawaambia, ufalme wa Mungu hauji kwa kuuchunguza; 21#Mt 24:23; Yn 1:26; 12:35 wala hawatasema, Tazama, upo huku, au, kule, kwa maana, tazama, ufalme wa Mungu umo ndani yenu.
22Akawaambia wanafunzi, Siku zitakuja mtakapotamani kuona siku moja katika siku zake Mwana wa Adamu, msiione. 23#Lk 21:8 Tena watawaambia, Tazama, kule! Tazama, huku! Msiondoke mahali mlipo, wala msiwafuate; 24#Mt 24:26,27 kwa kuwa, kama vile umeme umulikavyo toka upande huu chini ya mbingu hata upande huu chini ya mbingu, ndivyo atakavyokuwa Mwana wa Adamu katika siku yake. 25#Lk 9:22 Lakini kwanza, hana budi kupata mateso mengi, na kukataliwa na kizazi hiki. 26#Mwa 6:5-8; Mt 24:37-39 Na kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa katika siku zake Mwana wa Adamu. 27#Mwa 7:6-24 Walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakioa na kuolewa, hata siku ile Nuhu aliyoingia katika safina, gharika ikashuka ikawaangamiza wote. 28#Mwa 18:20—19:25 Na kadhalika, kama ilivyokuwa katika siku za Lutu, walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakinunua na kuuza, wakipanda na kujenga; 29#Mwa 19:24,25 lakini siku ile Lutu aliyotoka Sodoma kulinyesha moto na kibiriti kutoka mbinguni vikawaangamiza wote. 30Hivyo ndivyo itakavyokuwa siku ile atakayofunuliwa Mwana wa Adamu. 31#Mt 24:17-18; Mk 13:15-16; Mwa 19:26 Katika siku ile, aliye juu ya dari, na mali yake imo ndani ya nyumba, asishuke ili kuitwaa; na kadhalika, aliye shambani asirejee nyuma. 32#Mwa 19:26 Mkumbukeni mkewe Lutu. 33#Mt 10:39; 16:25; Mk 8:35; Lk 9:24; Yn 12:25 Mtu yeyote atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza; na yeyote atakayeiangamiza ataiponya. 34Nawaambia, usiku huo watu wawili watakuwa katika kitanda kimoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa. 35#Mt 24:40,41 Wanawake wawili watakuwa wakisaga pamoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa. [ 36Watu wawili watakuwa shambani, mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.] 37#Ayu 39:30; Mt 24:28 Wakajibu, wakamwuliza, Wapi, Bwana? Akawaambia, Ulipo mzoga, ndipo watakapokusanyika tai.

Iliyochaguliwa sasa

Luka 17: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha