Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mambo ya Walawi 18

18
Miiko ya ndoa
1BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 2#Kut 6:7; Eze 20:5 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu. 3#Eze 23:8; Kut 23:24 Nanyi msifanye matendo kama yale ya nchi ya Misri mlikokaa; wala msifanye matendo kama yale ya nchi ya Kanaani, nitakayowapeleka; wala msifuate amri zao hao. 4Mtayatii maagizo yangu, na mtazishika amri zangu, ili kuzifuata; mimi ndimi BWANA Mungu wenu. 5#Neh 9:29; Eze 18:9; 20:11-13; Lk 10:28; Rum 10:5; Gal 3:12; Isa 44:6; Yer 9:24; Mal 3:6 Kwa ajili ya hayo mtazishika amri zangu na maagizo yangu yeyote atakayefanya hivyo ataishi; mimi ndimi BWANA.
6Mtu yeyote miongoni mwenu asimkaribie mwenziwe aliye wa jamaa yake ya karibu ili kumfunua utupu; mimi ndimi BWANA. 7Utupu wa baba yako, wala utupu wa mama yako, usifunue, maana ndiye mama yako; usifunue utupu wake. 8#Law 20:11; Kum 22:30; 27:20; Mwa 49:4; 1 Kor 5:1 Utupu wa mke wa baba yako, usifunue; maana, ni utupu wa baba yako. 9#Law 20:17; Kum 27:22; 2 Sam 13:12 Utupu wa dada yako, binti ya baba yako, au binti ya mama yako, awe alizaliwa nyumbani mwenu au kwingine, utupu wa hao usifunue. 10Utupu wa binti ya mwanao wa kiume, au wa binti ya binti yako, utupu wao hao usifunue; kwa kuwa ni utupu wako mwenyewe. 11Utupu wa binti ya mkewe baba yako, aliyezaliwa na baba yako, yeye ni dada yako, usifunue utupu wake. 12#Law 20:19-20 Usifunue utupu wa dada ya baba yako; maana, yeye ni jamaa wa karibu. 13Usifunue utupu wa dada ya mama yako; maana, yeye ni jamaa ya mama yako wa karibu. 14Usifunue utupu wa ndugu ya baba yako, usimkaribie mkewe huyo; yeye ni shangazi yako. 15#Law 20:12; Mwa 38:18; Eze 22:11 Usifunue utupu wa mkweo mwanamke; yeye ni mke wa mwanao; usifunue utupu wake huyo. 16#Law 20:21; Mt 14:3,4; 22:24 Usifunue utupu wa mke wa nduguyo; maana, ni utupu wa nduguyo. 17#Law 20:14; Kum 27:23 Usifunue utupu wa mwanamke na binti yake; usimtwae binti ya mwanaye wa kiume, au binti ya binti yake, ili kufunua utupu wake; hao ni jamaa ya karibu; ni uovu mkuu. 18#Mwa 30:15; Mal 2:15 Wala usitwae#18:18 Au usimuoe. mwanamke pamoja na dada yake, awe mtesi wake, na kufunua utupu wake, dada yake akiwa hai. 19#Law 20:18; Eze 18:6 Usimwendee mwanamke kufunua utupu wake atakapokuwa najisi kwa ajili ya hedhi. 20#Law 20:10; Mit 6:29; Mal 3:5; Mt 5:27,28; 1 Kor 6:9; Ebr 13:4 Usilale na mke wa mwenzio, ukajitia unajisi naye. 21#Law 20:1-5; 2 Fal 16:3; Yer 19:5; 1 Fal 11:7,33; Eze 36:20; Mal 1:12; Isa 42:8 Usimtoe kafara mzawa wako yeyote kwa Moleki#18:21 Moleki ni jina la mungu aliyeabudiwa na Wakanaani, kwa kutoa dhabihu ya watoto wao kwa kuwapitisha motoni. Katika Agano Jipya ni Moloki. na ulinajisi jina la Mungu wako; mimi ndimi BWANA. 22#Law 20:13; Rum 1:27; 1 Tim 1:10 Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo. 23#Kut 22:18; Law 20:15-16; Kum 27:21 Wala usilale na mnyama yeyote, ili kujitia unajisi kwake; wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye; ni upotovu.
24 # Mt 15:18; 1 Kor 3:17; Kum 18:12 Msijitie unajisi katika hata mojawapo ya mambo hayo; kwa maana hayo mataifa nitakayoyatoa mbele zenu yamekuwa najisi kwa mambo hayo yote; 25#Hes 35:34; Isa 24:5; 26:21; Yer 9:9; 16:18 nayo nchi ikawa najisi; na nikaipatiliza kwa ajili ya uovu wake, kisha ikawatema wakazi wake. 26Kwa hiyo mtazishika amri zangu na maagizo yangu, wala msifanye mojawapo ya machukizo hayo; yeye aliye mzaliwa, wala mgeni aishiye kati yenu; 27(kwa kuwa hao watu wa nchi wameyafanya machukizo haya yote, hao waliotangulia mbele zenu, na hiyo nchi imekuwa najisi;) 28ili hiyo nchi isiwatapike na ninyi pia, hapo mtakapoitia unajisi, kama ilivyoitapika hiyo taifa iliyotangulia mbele yenu. 29Kwani mtu yeyote atakayefanya mojawapo ya machukizo hayo, nafsi hizo zitakazoyafanya zitakatiliwa mbali na watu wao. 30Kwa hiyo yafuateni maagizo yangu, ili kamwe msiwe na mojawapo ya tabia hizi zinazochukiza, zilizotangulia kufanywa mbele zenu; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.

Iliyochaguliwa sasa

Mambo ya Walawi 18: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha