Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mambo ya Walawi 15

15
Magonjwa ya zinaa
1Kisha BWANA akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia, 2#Law 22:4; Hes 5:2; 2 Sam 3:29; Mt 9:20; Mk 5:25; Lk 8:43 Haya, semeni na wana wa Israeli, mkawaambie, Mtu yeyote atakapokuwa na kisonono na kutokwa usaha mwilini mwake, atakuwa najisi kwa ajili ya kisonono chake. 3Na unajisi wake katika kisonono chake ni huu; kama mwili wake unachuruzika kisonono chake, au kama kisonono chake kimezuiwa mwilini mwake, ni unajisi wake. 4Kitanda chochote akilaliacho mwenye kisonono kitakuwa najisi; na kitu chochote atakachokalia kitakuwa najisi. 5#Law 11:25; 17:15; Ebr 9:10 Mtu yeyote atakayekigusa kitanda chake huyo, atazifua nguo zake, na kuoga mwili wake majini, naye atakuwa najisi hadi jioni. 6Na mtu atakayeketi katika kitu chochote alichokiketia mwenye kisonono, atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hadi jioni. 7Na mtu atakayegusa mwili wake mwenye kisonono atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hadi jioni. 8#Hes 12:8; Ayu 30:10; 2 Kor 7:1 Tena kama mwenye kisonono akimtemea mate mtu aliye safi; ndipo atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa ni najisi hadi jioni. 9Na tandiko lolote atakalolipanda mwenye kisonono litakuwa najisi. 10Mtu yeyote atakayegusa kitu chochote kilichokuwa chini yake huyo atakuwa najisi hadi jioni; na mtu atakayevichukua vitu vile atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hadi jioni. 11#1 Kor 15:33 Na mtu yeyote atakayeguswa na mwenye kisonono, ambaye hajanawa mikono yake majini, atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hadi jioni. 12#Law 6:28; 11:32,33 Na chombo cha udongo ambacho amekigusa mwenye kisonono, kitavunjwavunjwa; na kila chombo cha mti kitaoshwa majini. 13#Law 14:8; Hes 12:14; 19:11 Na huyo aliye na kisonono atakapotakaswa na kisonono chake, atajihesabia siku saba kwa kutakaswa kwake, naye atazifua nguo zake; naye ataoga mwili wake katika maji ya mtoni, naye atakuwa safi. 14#Law 14:22,23; Hes 6:10; Ebr 10:10-14 Na siku ya nane atajipatia hua wawili, au makinda mawili ya njiwa, naye atakwenda mbele za BWANA mlangoni pa hema ya kukutania, naye atampa kuhani hao ndege; 15#Law 14:30,31; 14:19,21; Ebr 9:14; 10:1 na kuhani atawasongeza, mmoja kuwa sadaka ya dhambi, na wa pili kuwa sadaka ya kuteketezwa; naye kuhani atafanya upatanisho mbele za BWANA kwa ajili ya kisonono chake.
16 # Law 22:4; 23:10 Na mtu yeyote akitokwa na shahawa yake, ndipo ataoga mwili wake wote majini, naye atakuwa najisi hadi jioni. 17Na kila nguo au ngozi, ambayo ina shahawa, itafuliwa kwa maji, nayo itakuwa najisi hata jioni. 18#1 Sam 21:4 Huyo mwanamke ambaye mwanamume amelala naye kwa shahawa, wote wawili wataoga majini, nao watakuwa najisi hadi jioni.
19 # Law 12:2; Eze 36:17 Mwanamke yeyote aliye na hedhi, atatengwa kwa muda wa siku saba; na mtu yeyote atakayemgusa atakuwa najisi hadi jioni. 20Na kitu chochote ambacho anakalia katika kutengwa kwake kitakuwa najisi; na kila kitu ambacho amekalia kitakuwa najisi. 21Mtu yeyote atakayekigusa kitanda chake huyo mwanamke atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hadi jioni. 22#2 Kor 7:1; Ebr 10:22 Mtu yeyote atakayekigusa chochote ambacho huyo mwanamke amekalia atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hadi jioni. 23Kiwe ni katika kitanda, au chochote alichokikalia huyo mwanamke, atakapokigusa kitu hicho, atakuwa najisi hadi jioni. 24#Law 20:18 Na mtu yeyote atakayelala na mwanamke na unajisi ukawa juu yake, atakuwa najisi muda wa siku saba; na kila kitanda alichokilalia kitakuwa najisi.
25 # Mt 9:20; Mk 5:25; Lk 8:43 Na mwanamke kama akitokwa na damu yake siku nyingi, nayo si katika majira ya kutengwa kwake, au kama anatoka damu kuzidi majira ya kutengwa kwake; siku hizo zote za kutoka damu ya unajisi wake, atakuwa kama alivyokuwa katika siku za kutengwa kwake; yeye ni najisi. 26Kila kitanda akilaliacho katika siku zote za kutoka damu kitakuwa kama kitanda cha kutengwa kwake; na kila kitu atakachokilalia kitakuwa najisi, kama unajisi wa kutengwa kwake. 27Na mtu yeyote atakayevigusa vitu vile atakuwa najisi, naye atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hadi jioni. 28Lakini huyo mwanamke akiwa ametakaswa na kule kutoka damu kwake, ndipo atakapojihesabia siku saba, na baadaye atakuwa safi. 29Siku ya nane atajipatia hua wawili, au makinda mawili ya njiwa, na kumletea kuhani, mlangoni pa hema ya kukutania. 30#Rum 3:25; 2 Kor 5:18,19; Efe 1:7; 2:12-22; Kol 1:19-22; Ebr 2:17; 9:14; 10:1; 1 Yoh 1:2,7; 2:1 Kuhani atamsongeza mmoja kuwa sadaka ya dhambi, na wa pili kuwa sadaka ya kuteketezwa; naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele za BWANA, kwa ajili ya kutoka damu ya unajisi kwake.
31 # Law 11:47; Kum 24:8; Eze 22:26; 44:23; Hes 5:3; 19:13,20; Eze 5:11; 23:38; 1 Kor 3:17 Ni hivi mtakavyowatenga wana wa Israeli na unajisi wao; ili wasife katika unajisi wao, hapo watakapoitia unajisi maskani yangu iliyo katikati yao.
32Hii ndiyo sheria ya mwenye kisonono, na ya mtu ambaye shahawa yake inamtoka, akawa na unajisi kwa ajili yake; 33na ya mwanamke ambaye yuko katika kutengwa kwake, na ya mtu ambaye ana kisonono, awe ni mwanamume, au ni mwanamke, na ya huyo alalaye na mwanamke mwenye unajisi.

Iliyochaguliwa sasa

Mambo ya Walawi 15: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha