Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yoshua 23

23
Yoshua awausia watu
1 # Yos 21:44; 22:4; 13:1 Hata ikawa baada ya siku nyingi, BWANA alipokuwa amekwisha kuwapa Israeli amani mbele ya adui zao pande zote, naye Yoshua alipokuwa mzee, mwenye miaka mingi sana, 2#Kum 31:28; Yos 24:1; 1 Nya 28:1 Yoshua akawaita Israeli wote, wazee wao, na wakuu wao, na waamuzi wao, na makamanda wao, akawaambia, Mimi ni mzee, nami nimezeeka sana; 3nanyi mmeona mambo yote ambayo BWANA, Mungu wenu, amewatenda mataifa haya yote kwa ajili yenu; kwa maana BWANA, Mungu wenu, ndiye aliyewapigania ninyi. 4Tazama, nimewagawieni kwa kura mataifa haya yaliyobaki, yawe urithi kwa makabila yenu, toka mto wa Yordani, pamoja na mataifa yote niliyowakatilia mbali, mpaka bahari kubwa upande wa magharibi. 5#Kut 23:30; 33:2; 34:11; Kum 11:23; Hes 33:53 Yeye BWANA, Mungu wenu, atawatoa kwa nguvu mbele yenu, atawafukuza wasiwe mbele ya macho yenu tena; nanyi mtaimiliki nchi yao, kama BWANA Mungu wenu, alivyowaambia. 6#Kum 5:32; 28:14 Basi, iweni thabiti sana kuyashika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha Torati ya Musa, na kuyatenda, msiyaache kwa kugeukia upande wa kulia wala upande wa kushoto. 7#Kut 23:33; Kum 7:2,3; Mit 4:14; Efe 5:11; Kut 23:13; Hes 32:38; Zab 16:4; Yer 5:7; Sef 1:5 Msiingie kati ya mataifa haya, yaani, haya yaliyobaki kati yenu; wala msitaje majina ya miungu yao, wala kuwaapisha watu kwa majina hayo, wala kuitumikia, wala kujiinamisha mbele yao; 8#Kum 10:20; 11:22 bali shikamaneni na BWANA, Mungu wenu, kama mlivyotenda mpaka hivi leo. 9#Yos 1:5 Maana BWANA amefukuza mbele yenu mataifa makuu na yenye nguvu, na kwenu ninyi hapana mtu aliyewahi kusimama mbele yenu hata leo. 10#Kum 3:22; 32:30; Amu 3:31; 15:15; 2 Sam 23:8 Mtu mmoja miongoni mwenu atafukuza watu elfu; maana BWANA, Mungu wenu, ndiye anayewapigania, kama alivyowaambia. 11Jihadharini nafsi zenu, basi, ili mmpende BWANA, Mungu wenu.
12 # Ebr 10:38; 2 Pet 2:20 Lakini mkirudi nyuma kwa njia yoyote na kushikamana na mabaki ya mataifa, yaani, mataifa haya yaliyobaki kati yenu, na kuoana nao, na kuingia kwao, nao kuingia kwenu; 13#Amu 2:3; 1 Fal 11:4 jueni hakika ya kuwa BWANA, Mungu wenu, hatawafukuza tena mataifa haya mbele ya macho yenu, bali watakuwa mtego kwenu na tanzi, na mjeledi mbavuni mwenu, na miiba machoni mwenu, hadi mtakapoangamia na kutoka katika nchi hii njema, ambayo BWANA, Mungu wenu, amewapa ninyi. 14#Mhu 12:3-7; Ebr 9:27; 11:13; Lk 21:33 Angalieni, mimi leo ninakwenda njia ile waendayo watu wote wa ulimwengu; nanyi nyote mnajua mioyoni mwenu, na rohoni mwenu, ya kuwa halikuwapungukia ninyi hata neno moja katika mambo hayo mema yote aliyoyanena BWANA, Mungu wenu, katika habari zenu; yote yametimia kwenu hapana neno lolote mlilopungukiwa. 15#Kum 28:63; Law 26:16; Kum 28:15,16; Amu 3:8,12; 4:1; Lk 21:22 Kisha itakuwa, kama yalivyowafikia yale mambo mema yote, BWANA, Mungu wenu, aliyowaahidia ninyi, kadhalika BWANA atawafikilizia mabaya yote, hata atakapokuwa amewaangamiza katika nchi hii njema, BWANA Mungu wenu, aliyowapa. 16Hapo mtakapolivunja agano la BWANA, Mungu wenu, alilowaamuru, na kwenda kuitumikia miungu mingine, na kujiinamisha mbele yao, ndipo hasira ya BWANA itakapowaka juu yenu, nanyi mtaangamia upesi katika nchi hii njema aliyowapa.

Iliyochaguliwa sasa

Yoshua 23: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha