Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Waraka kwa Waebrania 5

5
1Maana kila kuhani mkuu aliyetwaliwa katika wanadamu amewekwa kwa ajili ya wanadamu katika mambo yanayomhusu Mungu, ili atoe matoleo na dhabihu kwa ajili ya dhambi; 2#Ebr 4:15 awezaye kuwachukulia kwa upole wao wasiojua na wenye kupotea, kwa kuwa yeye mwenyewe ana udhaifu; 3#Law 9:7; 16:6 na kwa sababu hiyo imempasa, kama kwa ajili ya watu, vivyo hivyo kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi. 4#Kut 28:1 Na hapana mtu ajitwaliaye mwenyewe heshima hii, ila yeye aitwaye na Mungu, kama vile Haruni. 5#Zab 2:7; Mdo 13:33 Vivyo hivyo Kristo naye hakujitukuza nafsi yake kufanywa kuhani mkuu, lakini yeye aliyemwambia,
Ndiwe mwanangu,
Mimi leo nimekuzaa.
6 # Zab 110:4; Ebr 7:1 Kama asemavyo mahali pengine,
Ndiwe kuhani milele
Kwa mfano wa Melkizedeki.
7 # Mt 26:36-46; Mk 14:32-42; Lk 22:39-46 Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu; 8#Flp 2:8 na, ingawa ni Mwana, alijifunza kutii kwa mateso hayo yaliyompata; 9#Isa 45:17; Yn 17:1,5 naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii; 10kisha ametajwa na Mungu kuwa kuhani mkuu kwa mfano wa Melkizedeki.
Maonyo juu ya uasi
11Yeye ambaye tuna maneno mengi ya kunena kuhusu habari zake; na ni shida kuyaeleza kwa kuwa mmekuwa wavivu wa kusikia. 12#1 Kor 3:2; 1 Pet 2:2 Kwa maana, iwapasapo kuwa waalimu, (maana wakati mwingi umepita), mnahitaji kufundishwa na mtu mafundisho ya kwanza ya maneno ya Mungu; nanyi mmekuwa mnahitaji maziwa wala si chakula kigumu. 13#Efe 4:14 Kwa maana kila mtu atumiaye maziwa hajui sana neno la haki, kwa kuwa ni mtoto mchanga. 14#Flp 1:10; Rum 16:19; Mwa 2:17 Lakini chakula kigumu ni cha watu wazima, ambao akili zao, kwa kutumiwa, zimezoeshwa kupambanua mema na mabaya.

Iliyochaguliwa sasa

Waraka kwa Waebrania 5: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha