Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwanzo 18

18
Abrahamu na Sara waahidiwa mtoto
1 # Mwa 13:18; 14:13; Mdo 7:2 BWANA akamtokea Abrahamu karibu na mialoni ya Mamre, alipokuwa ameketi mlangoni pa hema yake mchana wakati wa joto. 2#Ebr 13:2; Mwa 18:22; 19:1; 1 Pet 4:9 Akainua macho yake akaona, na tazama, watu watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga mbio kuwalaki kutoka mlangoni pa hema, akainama mpaka chini, 3akasema, Bwana wangu, kama nimeona fadhili machoni pako nakuomba usinipite sasa mimi mtumwa wako. 4#Mwa 24:32; 43:24 Na yaletwe basi maji kidogo mkanawe miguu, mkapumzike chini ya mti huu. 5Nami nitaleta chakula kidogo, mkaburudishe moyo, baadaye mwendelee, kwa maana mmemjia mtumwa wenu. Wakasema, Haya, fanya kama ulivyosema.
6Basi Abrahamu akaenda hima hemani kwa Sara, akasema, Tayarisha haraka vipimo vitatu vya unga safi, uukande, ufanye mikate. 7Abrahamu akapiga mbio kwenda kundini, akaleta ndama wa ng'ombe aliye laini, mzuri, akampa mtumishi, naye akaharakisha kuiandaa. 8Akatwaa siagi na maziwa, na ndama aliyoiandaa, akawaandalia mbele yao, akasimama karibu nao chini ya mti, nao wakala.
9 # Mwa 24:67; Tit 2:5 Wakamwambia, Yu wapi Sara mkeo? Akasema, Yumo hemani. 10#Rum 9:9; Mwa 21:2; Lk 1:13 Akamwambia, Hakika nitakurudia wakati huu huu mwakani, na tazama, Sara mkeo atapata mwana wa kiume. Sara akasikia mlangoni pa hema iliyokuwapo nyuma yake. 11#Rum 4:19; Ebr 11:11 Basi Abrahamu na Sara walikuwa wazee wenye umri mkubwa, na Sara alikuwa amekoma katika desturi ya wanawake. 12#1 Pet 3:6; Lk 1:18; Mwa 17:17 Kwa hiyo Sara akacheka moyoni mwake, akisema, Niwapo mkongwe, nitapata furaha, na bwana wangu mzee? 13BWANA akamwambia Abrahamu, Mbona Sara amecheka akisema, Mimi kweli nitazaa mwana, nami ni mzee? 14#Lk 1:37; Zab 115:3; Yer 32:17; Zek 8:6; Mt 3:9; 19:26; Rum 4:21; Ebr 11:19 Kuna neno gani lililo gumu la kumshinda BWANA? Kwa muhula wake nitakurudia, wakati huu huu mwakani, na Sara atapata mwana wa kiume. 15Akakana Sara, akisema, Sikucheka, maana aliogopa. Naye akasema, Sivyo! Umecheka.
Abrahamu aombea Sodoma
16Kisha watu hao wakaondoka huko wakaelekeza nyuso zao Sodoma. Abrahamu akaenda pamoja nao awasindikize. 17#Zab 25:14; Amo 3:7; Yn 15:15 BWANA akasema, Je! Nimfiche Abrahamu jambo ambalo ninataka kulifanya, 18#Mwa 12:3; 22:18; Zab 72:17; Mdo 3:25; Gal 3:8,9,16,18 ikiwa Abrahamu atakuwa taifa kuu, hodari, na katika yeye mataifa yote ya dunia watabarikiwa? 19#Kum 6:6,7; Yos 24:15; Efe 6:4 Kwa maana nimemchagua#18:19 Nimemchagua: Katika Kiebrania ni nimemjua. ili awaamuru wanawe na vizazi vyake baada yake wadumishe njia ya BWANA, kwa kuwa wenye haki na kweli, ili BWANA naye akamtimizie Abrahamu ahadi zake. 20#Mwa 4:10; 19:13; Yak 5:4 BWANA akasema, Kwa kuwa kilio cha Sodoma na Gomora kimezidi, na dhambi zao zimeongezeka sana, 21#Mwa 11:5; Kut 3:8; Zab 14:2; Ebr 4:13 basi, nitashuka sasa nione kama wanayotenda ni kiasi cha kilio kilichonijia; na kama sivyo, nitajua. 22#Mwa 18:1,2 Basi wale watu wakatoka huko wakaelekea Sodoma; lakini Abrahamu alibaki amesimama mbele za BWANA.
23 # Hes 16:22; 2 Sam 24:17; Zab 11:4-7 Abrahamu akakaribia, akasema, Je! Utaharibu mwenye haki pamoja na mwovu? 24#Mt 7:13,14 Huenda wakawapo wenye haki hamsini katika mji, utaharibu, wala hutauacha mji kwa ajili ya hao hamsini wenye haki waliomo? 25#Isa 3:10,11; Ayu 8:3,20; Zab 58:11; 94:2; Rum 3:5,6 La hasha! Usifanye hivyo, ukamwue mwenye haki pamoja na mwovu, mwenye haki awe kama mwovu. Hasha! Mhukumu ulimwengu wote asitende haki? 26#Yer 5:1; Eze 22:30; Mt 24:22 BWANA akasema, Nikiona katika Sodoma wenye haki hamsini mjini, nitapaacha mahali pote kwa ajili yao.
27 # Lk 18:1; Zab 8:4 Abrahamu akajibu, akasema, Basi, nimeshika kusema na Bwana, nami ni mavumbi na majivu tu. 28Huenda wakapunguka watano katika wale hamsini wenye haki, je! Utaharibu mji wote kwa kupungua watano? Akasema, Sitauharibu, nikiona humo arubaini na watano. 29#1 The 5:17 Akazidi tena kusema naye, akinena, Huenda wakaonekana humo arubaini? Akasema, Sitafanya kwa ajili ya hao arubaini.
30 # Isa 55:8,9 Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami nitasema, Huenda wakaonekana huko thelathini? Akasema, Sitafanya, nikiona humo thelathini. 31#Ebr 4:16 Akasema, Tazama, nimeshika kusema na Bwana, huenda wakaonekana huko ishirini? Akasema, Sitaharibu kwa ajili ya hao ishirini. 32#Amu 6:39; Kut 34:6,7; Zab 34:15; Mit 15:29; 1 Yoh 3:22; Yak 5:16 Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami nitasema mara hii tu, Huenda wakaonekana huko kumi? Akasema, Sitaharibu kwa ajili ya hao kumi. 33Basi BWANA alipokwisha kuzungumza na Abrahamu, akaenda zake; Abrahamu naye akarudi mahali pake.

Iliyochaguliwa sasa

Mwanzo 18: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha