Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Wakolosai 4

4
1 # Efe 6:9; Law 25:43,53 Ninyi akina bwana, wapeni watumishi wenu yaliyo haki na ya adili, mkijua ya kuwa ninyi nanyi mna Bwana mbinguni.
Maagizo zaidi
2 # 1 The 5:17; Efe 6:18; Flp 4:6 Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba mkiwa na shukrani; 3#Rum 15:30; Efe 6:18,19; 2 The 3:1; 1 Kor 16:9 mkituombea na sisi pia, kwamba Mungu atufungulie mlango kwa lile neno lake, tuinene siri ya Kristo, ambayo kwa ajili yake nimefungwa, 4#Efe 6:20 ili niidhihirishe, kama inipasavyo kunena. 5#Efe 5:15,16; 1 The 4:12 Nendeni kwa hekima mbele yao walio nje, mkiukomboa wakati. 6#Efe 4:29; Mk 9:50; 1 Pet 3:15 Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolezwa chumvi, ili mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu.
Salamu za mwisho na baraka
7 # Mdo 20:4; 2 Tim 4:12; Efe 6:21 Tikiko, ndugu mpendwa, mtumishi mwaminifu, mwenzi wangu katika Bwana, atawaarifu mambo yangu yote; 8#Efe 6:22 ambaye nimemtuma kwenu kwa sababu iyo hiyo, ili mjue mambo yetu, naye akawafariji mioyo yenu; 9#Flm 1:10-12 pamoja na Onesimo, ndugu mwaminifu, mpendwa, aliye mtu wa kwenu. Hao watawaarifu mambo yote ya hapa petu.
10 # Mdo 12:12,25; 13:13; 15:37-39; 18:27; 19:29; 27:2; Flm 1:24 Aristarko, aliyefungwa pamoja nami, awasalimu; pamoja na Marko, binamu yake Barnaba, ambaye mmepokea maagizo juu yake; akifika kwenu mkaribisheni. 11Na Yesu#4:11 Katika makala zingine ni Yoshua. aitwaye Yusto awasalimu. Hao tu ndio watu wa tohara miongoni mwa wale watendao kazi pamoja nami kwa ajili ya ufalme wa Mungu; nao wamekuwa msaada kwangu. 12#Kol 1:7; Flm 1:23 Epafra, aliye mtu wa kwenu, mtumwa wa Yesu Kristo, awasalimu, akifanya bidii siku zote kwa ajili yenu katika maombi yake, ili msimame mkiwa wakamilifu na kuthibitika kabisa katika mapenzi yote ya Mungu. 13Maana namshuhudia kwamba ana juhudi nyingi kwa ajili yenu, na kwa ajili ya hao walioko Laodikia, na kwa ajili ya hao walioko Hierapoli. 14#2 Tim 4:10,11; Flm 1:24 Luka, yule tabibu mpendwa, na Dema, wanawasalimu. 15Wasalimuni ndugu walioko Laodikia, na Nimfa, na kanisa lililo katika nyumba yake. 16Waraka huu ukiisha kusomwa kwenu hakikisheni kwamba unasomwa katika kanisa la Walaodikia pia; na ule wa Laodikia usomwe na ninyi. 17#Flm 1:2 Mwambieni Arkipo, Iangalie sana huduma ile uliyopewa katika Bwana, ili uitimize.
18 # 1 Kor 16:21; 2 The 3:17 Naandika salamu yangu mimi Paulo, kwa mkono wangu mwenyewe. Kumbukeni kufungwa kwangu. Neema na iwe pamoja nanyi.

Iliyochaguliwa sasa

Wakolosai 4: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha