Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ufu 22

22
Mto wa Maji ya Uzima
1 # Eze 47:1; Zek 14:8 Kisha akanionyesha mto wa maji ya uzima, wenye kung’aa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana-Kondoo, 2#Mwa 2:9; Eze 47:12; Ufu 21:21katikati ya njia kuu yake. Na upande huu na upande huu wa ule mto, ulikuwapo mti wa uzima, uzaao matunda, aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa. 3#Zek 14:11Wala hapatakuwa na laana yo yote tena. Na kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-Kondoo kitakuwamo ndani yake. Na watumwa wake watamtumikia; 4#Mt 5:8; Ufu 3:12nao watamwona uso wake, na jina lake litakuwa katika vipaji vya nyuso zao. 5#Isa 60:19; Dan 7:18,27; Ufu 21:25Wala hapatakuwa na usiku tena; wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu huwatia nuru, nao watatawala hata milele na milele.
6 # Ufu 1:1; 1 Kor 14:32 Kisha akaniambia, Maneno haya ni amini na kweli. Naye Bwana, Mungu wa roho za manabii, alimtuma malaika wake kuwaonyesha watumwa wake mambo ambayo hayana budi kuwako upesi. 7#Ufu 3:11; 1:3Na tazama, naja upesi; heri yeye ayashikaye maneno ya unabii wa kitabu hiki.
Hitimisho na Baraka
8 # Ufu 19:10 Nami Yohana ndimi niliyeyasikia na kuyaona mambo hayo. Na hapo nilipoyasikia na kuyaona nalianguka, ili nisujudu mbele ya miguu ya malaika yule mwenye kunionyesha hayo. 9Naye akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni mjoli wako, na wa ndugu zako manabii, na wa wale wayashikao maneno ya kitabu hiki. Msujudie Mungu.
10 # Ufu 10:4; 1:3; Dan 8:26; 12:4 Akaniambia, Usiyatie muhuri maneno ya unabii wa kitabu hiki, kwa maana wakati huo umekaribia. 11#Dan 12:10Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa. 12#Isa 40:10; 62:11; Zab 28:4; 62:12; Yer 17:10; Ufu 3:11; Rum 2:6Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. 13#Ufu 1:8,17; 2:8; Isa 44:6; 48:12; Ebr 13:8Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho. 14#Mwa 2:9; 3:22; 49:11Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake. 15#Ufu 21:8,27; 1 Kor 6:9,10Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.
16 # Isa 11:1,2,10; 5:5; Isa 11:1,10; Lk 1:78; Ufu 1:1,2; 5:5 Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung’aa ya asubuhi.
17 # Isa 55:1; Ufu 21:6; Zek 14:8; Rum 8:23; Yn 7:37 Na Roho na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure.
18 # Kum 4:2; 12:32; 29:20; Ufu 15:1,6 Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki. 19#Mwa 2:9; 3:22Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.
20Yeye mwenye kuyashuhudia haya asema, Naam; naja upesi. Amina; na uje, Bwana Yesu.
21Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi nyote. Amina.

Iliyochaguliwa sasa

Ufu 22: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha