Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 45

45
Wimbo wa Arusi ya Kifalme
Kwa mwimbishaji: kwa kufuata mtindo wa Yungiyungi. Wimbo wa Wakorahi; Wimbo wa Mapenzi.
1Moyo wangu umefurika kwa neno jema,
Mimi nasema niliyomfanyizia mfalme;
Ulimi wangu ni kalamu ya mwandishi mstadi.
2Wewe u mzuri sana kuliko wanadamu;
Neema imemiminiwa midomoni mwako,
Kwa hiyo Mungu amekubariki hata milele.
3Jifungie upanga wako pajani, wewe uliye hodari,
Utukufu ni wako na fahari ni yako.
4Katika fahari yako usitawi uendelee
Kwa ajili ya kweli na upole na haki
Na mkono wako wa kuume
Utakufundisha mambo ya kutisha.
5Mishale yako ni mikali, watu huanguka chini yako;
Imo mioyoni mwa adui za mfalme.
6 # Ebr 1:8-9; Zab 93:2; Isa 9:6,7 Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele,
Fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili.
7 # Zab 33:5; Mt 3:15; Ebr 1:9; Isa 61:1; Yn 20:17 Umeipenda haki;
Umeichukia dhuluma.
Kwa hiyo MUNGU, Mungu wako, amekupaka mafuta,
Mafuta ya furaha kuliko wenzako.
8Mavazi yako yote hunukia manemane
Na udi na mdalasini.
Katika majumba ya pembe
Vinubi vimekufurahisha.
9Binti za wafalme wamo
Miongoni mwa akina bibi wako wastahiki.
Mkono wako wa kuume amesimama malkia
Amevaa dhahabu ya Ofiri.
10 # Kum 21:13 Sikia, binti, utazame, utege sikio lako,
Uwasahau watu wako na nyumba ya baba yako.
11 # Zab 95:6; Isa 54:5 Naye mfalme atautamani uzuri wako,
Maana ndiye bwana wako, nawe umsujudie.
12Na binti Tiro analeta kipawa chake,
Nao matajiri wa watu watajipendekeza kwako.
13 # Ufu 19:7,8 Binti mfalme yumo ndani ana fahari tupu,
Mavazi yake ni ya nyuzi za dhahabu.
14Atapelekwa kwa mfalme
Na mavazi yaliyofumwa kwa uzuri.
Wanawali wenzake wanaomfuata,
Watapelekwa kwako.
15Watapelekwa kwa furaha na shangwe,
Na kuingia katika nyumba ya mfalme.
16 # 1 Pet 2:9; Ufu 1:6 Badala ya baba zako watakuwapo watoto wako,
Utawafanya kuwa wakuu katika nchi zote.
17 # Isa 11:10; Mal 1:11 Jina lako nitalifanya kuwa kumbukumbu
Katika vizazi vyote.
Kwa hiyo mataifa watakushukuru
Milele na milele.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 45: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha