Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 18:1-24

Zab 18:1-24 SUV

Wewe, BWANA, nguvu zangu, nakupenda sana; BWANA ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia, Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu. Nitamwita BWANA astahiliye kusifiwa, Hivyo nitaokoka na adui zangu. Kamba za mauti zilinizunguka, Mafuriko ya uovu yakanitia hofu. Kamba za kuzimu zilinizunguka, Mitego ya mauti ikanikabili. Katika shida yangu nalimwita BWANA, Na kumlalamikia Mungu wangu. Akaisikia sauti yangu hekaluni mwake, Kilio changu kikaingia masikioni mwake. Ndipo nchi iliyotikisika na kutetemeka, Misingi ya milima ikasuka-suka; Ikatikisika kwa sababu alikuwa na ghadhabu. Kukapanda moshi kutoka puani mwake, Moto ukatoka kinywani mwake ukala, Makaa yakawashwa nao. Aliziinamisha mbingu akashuka, Kukawa na giza kuu chini ya miguu yake. Akapanda juu ya kerubi akaruka, Naam, aliruka upesi juu ya mabawa ya upepo. Alifanya giza kuwa mahali pake pa kujificha, Kuwa hema yake ya kumzunguka. Giza la maji na mawingu makuu ya mbinguni. Toka mwangaza uliokuwa mbele zake Kukapita mawingu yake makuu. Mvua ya mawe na makaa ya moto. BWANA alipiga radi mbinguni, Yeye Aliye juu akaitoa sauti yake, Mvua ya mawe na makaa ya moto. Akaipiga mishale yake akawatawanya, Naam, umeme mwingi sana, akawatapanya. Ndipo ilipoonekana mikondo ya maji, Misingi ya ulimwengu ikafichuliwa, Ee BWANA, kwa kukemea kwako, Kwa mvumo wa pumzi ya puani mwako. Alipeleka kutoka juu akanishika, Na kunitoa katika maji mengi. Akaniokoa na adui yangu mwenye nguvu, Na wale walionichukia, Maana walikuwa na nguvu kuliko mimi. Walinikabili siku ya msiba wangu, Lakini BWANA alikuwa tegemeo langu. Akanitoa akanipeleka panapo nafasi, Aliniponya kwa kuwa alipendezwa nami. BWANA alinitendea sawasawa na haki yangu, Sawasawa na usafi wa mikono yangu akanilipa. Maana nimezishika njia za BWANA, Wala sikumwasi Mungu wangu. Hukumu zake zote zilikuwa mbele yangu, Wala amri zake sikujiepusha nazo. Nami nalikuwa mkamilifu mbele zake, Nikajilinda na uovu wangu. Mradi BWANA amenilipa sawasawa na haki yangu, Sawasawa na usafi wa mikono yangu mbele zake.

Soma Zab 18

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zab 18:1-24

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha