Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 119:17-24

Zab 119:17-24 SUV

Umtendee mtumishi wako ukarimu, Nipate kuishi, nami nitalitii neno lako. Unifumbue macho yangu niyatazame Maajabu yatokayo katika sheria yako. Mimi ni mgeni katika nchi, Usinifiche maagizo yako. Roho yangu imepondeka kwa kutamani Hukumu zako kila wakati. Umewakemea wenye kiburi, Wamelaaniwa waendao mbali na maagizo yako. Uniondolee laumu na dharau, Kwa maana nimezishika shuhuda zako. Wakuu nao waliketi wakaninena, Lakini mtumishi wako atazitafakari amri zako. Shuhuda zako nazo ndizo furaha yangu, Na washauri wangu.

Soma Zab 119

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha