Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 119:1-8

Zab 119:1-8 SUV

Heri walio kamili njia zao, Waendao katika sheria ya BWANA. Heri wazitiio shuhuda zake, Wamtafutao kwa moyo wote. Naam, hawakutenda ubatili, Wamekwenda katika njia zake. Wewe umetuamuru mausia yako, Ili sisi tuyatii sana. Ningependa njia zangu ziwe thabiti, Nizitii amri zako. Ndipo mimi sitaaibika, Nikiyaangalia maagizo yako yote. Nitakushukuru kwa unyofu wa moyo, Nikiisha kujifunza hukumu za haki yako Nitazitii amri zako, Usiniache kabisa

Soma Zab 119

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zab 119:1-8

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha