Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Law 18

18
Miiko ya Ndoa
1BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 2#Kut 6:7; Eze 20:5Nena wewe na wana wa Israeli, uwaambie, Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu. 3#Eze 23:8; Kut 23:33Nanyi msifanye matendo kama yale ya nchi ya Misri mliyokaa; wala msifanye matendo kama yale ya nchi ya Kanaani, nitakayowapeleka; wala msiende katika amri zao hao. 4Mtazifanya hukumu zangu, nanyi mtazishika amri zangu, ili mwenende katika hizo; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu. 5#Neh 9:29; Eze 18:9; 20:11-13; Lk 10:28; Rum 10:5; Gal 3:12; Isa 44:6; Yer 9:24; Mal 3:6Kwa ajili ya hayo mtazishika amri zangu na hukumu zangu; ambazo mtu akizitumia ataishi kwa hizo; mimi ndimi BWANA.
6Mtu ye yote aliye wa kwenu asimkaribie mwenziwe aliye wa jamaa yake ya karibu ili kumfunua utupu; mimi ndimi BWANA. 7Utupu wa baba yako, wala utupu wa mama yako, usifunue, maana ndiye mama yako; usifunue utupu wake. 8#Law 20:11; Kum 22:30; 27:20; Mwa 49:4; 1 Kor 5:1Utupu wa mke wa baba yako, usifunue; maana, ni utupu wa baba yako. 9#Law 20:17; Kum 27:22; 2 Sam 13:12Utupu wa umbu lako, binti ya baba yako, au binti ya mama yako, kwamba alizaliwa nyumbani mwenu au kwamba alizaliwa kwengine, utupu wa hao usifunue. 10Utupu wa binti ya mwanao mume, au wa binti ya binti yako, utupu wao hao usifunue; kwa kuwa ndio utupu wako mwenyewe. 11Utupu wa binti ya mkewe baba yako, aliyezaliwa na baba yako, yeye ni umbu lako, usifunue utupu wake. 12#Law 20:19-20Usifunue utupu wa umbu lake baba yako; maana, yeye ni jamaa aliye karibu. 13Usifunue utupu wa umbu la mama yako; maana, yeye ni jamaa ya mama yako ya karibu. 14Usifunue utupu wa ndugu ya baba yako, usimkaribie mkewe huyo; yeye ni shangazi lako. 15#Law 20:12; Mwa 38:18; Eze 22:11Usifunue utupu wa mkweo mwanamke; yeye ni mke wa mwanao; usifunue utupu wake huyo. 16#Law 20:21; Mt 14:3,4; 22:24Usifunue utupu wa mke wa nduguyo; maana, ni utupu wa nduguyo. 17#Law 20:14; Kum 27:23Usifunue utupu wa mwanamke na binti yake; usimtwae binti ya mwanawe mume, au binti ya binti yake, ili kufunua utupu wake; hao ni jamaa ya karibu; ni uovu mkuu. 18#Mwa 30:15; Mal 2:15Wala usitwae mwanamke pamoja na nduguye, awe mtesi wake, na kufunua utupu wake, huyo wa pili atakapokuwa yu hai. 19#Law 20:18; Eze 18:6Nawe usimkaribie mwanamke kufunua utupu wake wakati wa kutengwa kwa ajili ya unajisi wake. 20#Law 20:10; Mit 6:29; Mal 3:5; Mt 5:27,28; 1 Kor 6:9; Ebr 13:4Usilale na mke wa mwenzio, ukajitia unajisi naye. 21#Law 20:1-5; 2 Fal 16:3; Yer 19:5; 1 Fal 11:7,33; Eze 36:20; Mal 1:12; Isa 42:8Nawe usitoe kizazi chako cho chote na kuwapisha kwa Moleki, wala usilinajisi jina la Mungu wako; mimi ndimi BWANA. 22#Law 20:13; Rum 1:27; 1 Tim 1:10Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo. 23#Kut 22:18; Law 20:15-16; Kum 27:21Wala usilale na mnyama ye yote, ili kujitia unajisi kwake; wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye; ni uchafuko.
24 # Mt 15:18; 1 Kor 3:17; Kum 18:12 Msijitie unajisi katika mambo hayo hata mojawapo; kwa maana hizo taifa nitakazozitoa mbele zenu zimekuwa najisi kwa mambo hayo yote; 25#Hes 35:34; Isa 24:5; 26:21; Yer 9:9; 16:18na hiyo nchi imekuwa najisi; kwa ajili ya hayo naipatiliza uovu wake juu yake, na hiyo nchi yatapika wenyeji wake na kuwatoa. 26Kwa hiyo mtazishika amri zangu na hukumu zangu, wala msifanye machukizo hayo mojawapo; yeye aliye mzalia, wala mgeni aketiye kati yenu; 27(kwa kuwa hao watu wa nchi wameyafanya machukizo haya yote, hao waliotangulia mbele zenu, na hiyo nchi imekuwa najisi;) 28ili kwamba hiyo nchi isiwatapike na ninyi pia, hapo mtakapoitia unajisi, kama ilivyoitapika hiyo taifa iliyotangulia mbele yenu. 29Kwani mtu awaye yote atakayefanya machukizo hayo mojawapo, nafsi hizo zitakazoyafanya zitakatiliwa mbali na watu wao. 30Kwa ajili ya hayo yashikeni mausia yangu, ili kwamba msifanye kabisa desturi hizi zichukizazo mojawapo, zilizotangulia kufanywa mbele zenu, wala msijitie unajisi katika mambo hayo; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.

Iliyochaguliwa sasa

Law 18: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha