Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yud UTANGULIZI

UTANGULIZI
Mwandishi wa Waraka huu mfupi huaminiwa kuwa ni nduguye Yesu Kristo na Yakobo. Mapokeo ya Kanisa husema kuwa alikuwa kiongozi wa kanisa baada ya kifo cha Yakobo. Waraka wa Yuda unahesabiwa kati ya “Nyaraka kwa Watu Wote” (tazama utangulizi kwa Waraka wa Yakobo).
Kwa sehemu kubwa Waraka huu unahusu masuala yale yale yanayoshughulikiwa na ule Waraka wa Pili wa Petro. Makusudi yake ni kupinga mafundisho ya uongo ya watu walioleta migawanyiko katika jumuiya ya Kikristo yenye misingi ya ujuzi fulani. Mafundisho hayo yalisema kwamba mwenye uzoefu wa hali ya juu katika maisha ya kiroho akifanya dhambi yoyote ile haigusi usafi wa roho yake. Anasa, uzinzi na uasherati vilihesabiwa kuwa alama ya kukomaa kiroho (aya 4,6-8,12-13,16). Waraka unawahakikishia waumini kwamba hukumu ya Mungu itawakabili watu hao. Kwa upande mwingine, mwandishi anawataka Wakristo wajaribu kuwaokoa wale walio dhaifu na hata kuwaonyesha huruma watu ambao maisha yao maovu yanakataliwa na Wakristo (22-23).

Iliyochaguliwa sasa

Yud UTANGULIZI: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha