Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yer 50

50
Hukumu Dhidi ya Babeli
1 # Isa 13:1; 21:1 Neno hili ndilo alilosema BWANA, katika habari za Babeli, na katika habari za Wakaldayo, kwa kinywa cha Yeremia, nabii.
2 # Isa 46:1; Yer 43:12 Tangazeni katika mataifa,
Mkahubiri na kutweka bendera;
Hubirini, msifiche, semeni,
Babeli umetwaliwa!
Beli amefedheheka;
Merodaki amefadhaika;
Sanamu zake zimeaibishwa,
Vinyago vyake vimefadhaika.
3 # Isa 13:17 Maana toka kaskazini taifa linakuja juu yake, litakaloifanya nchi yake kuwa ukiwa; wala hapana mtu atakayekaa humo; wamekimbia, wamekwenda zao, mwanadamu na mnyama pia. 4#Hos 1:11; 3:5; Zab 126:5; 105:4; Zek 12:10; 8:21,22; Isa 45:19Katika siku hizo, na wakati huo, asema BWANA, wana wa Israeli watakuja, wao na wana wa Yuda pamoja; Wataendelea njiani mwao wakilia, nao watamtafuta BWANA, Mungu wao. 5#Yer 31:31; 1 Pet 2:25Watauliza habari za Sayuni, na nyuso zao zitaelekea huko, wakisema, Njoni ninyi, mjiunge na BWANA, kwa agano la milele ambalo halitasahauliwa.
6Watu wangu wamekuwa kondoo waliopotea, wachungaji wao wamewapoteza; wamewapotosha milimani; wamekwenda toka mlima hata kilima, wamesahau mahali pao pa kupumzika. 7#Zek 11:5; Yer 2:3; Dan 9:16; Zab 22:4Watu wote waliowaona wamewala; na adui zao walisema, Sisi hatuna hatia, kwa kuwa hao wametenda dhambi juu ya BWANA, aliye kao la haki, yaani, BWANA, tumaini la baba zao. 8#Ufu 18:4; Isa 48:20; Yer 51:6; Zek 2:6Kimbieni kutoka kati ya Babeli, mkatoke katika nchi ya Wakaldayo, mkawe kama mabeberu mbele ya makundi. 9Kwa maana juu ya Babeli nitaamsha na kuleta kusanyiko la mataifa makubwa, toka nchi ya kaskazini; nao watajipanga juu yake; kutoka huko atatwaliwa; mishale yao itakuwa kama ya mtu shujaa aliye stadi; hapana hata mmoja utakaorudi bure. 10#Ufu 17:16Nao Ukaldayo utakuwa mateka; wote wautekao watashiba, asema BWANA. 11#Isa 47:6Kwa sababu mnafurahi, kwa sababu mnashangilia, enyi mnaouteka urithi wangu, kwa sababu mmewanda kama mtamba akanyagaye nafaka, nanyi mnalia kama farasi wenye nguvu; 12mama yenu atatahayarika sana; yeye aliyewazaa atafadhaika; tazama, atakuwa taifa lililo nyuma katika mataifa yote, atakuwa jangwa, nchi ya ukame, na nyika. 13Kwa sababu ya ghadhabu ya BWANA haitakaliwa na mtu, bali itakuwa ukiwa mtupu; kila mtu apitaye karibu na Babeli atashangaa, atazomea kwa sababu ya mapigo yake yote.
14Jipangeni juu ya Babeli pande zote,
Ninyi nyote mpindao upinde;
Mpigeni, msiuzuie hata mshale mmoja;
Kwa maana amemtenda BWANA dhambi.
15 # 1 Nya 29:24; 2 Nya 30:8; Omb 5:6; Yer 51:58; Zab 2:1-3; Ufu 16:6 Mpigieni kelele pande zote; amejitoa;
Maboma yake yameanguka, kuta zake zimebomolewa;
Kwa maana ni kisasi cha BWANA; mlipizeni kisasi;
Kama yeye alivyotenda, mtendeni yeye.
16 # Isa 13:14 Mpanzi mkatilie mbali na Babeli,
Naye ashikaye mundu wakati wa mavuno;
Kwa sababu ya kuuogopa upanga uoneao,
Watageuka kila mtu kwa watu wake,
Nao wataikimbilia kila mmoja nchi yake.
17 # Yoe 3:12; Mt 9:36; Yer 23:2; 2:15; 1 Pet 2:25; 2 Nya 28:20; 2 Fal 17:6; 24:10,14; Isa 7:17,20; 8:7,8 Israeli ni kondoo aliyetawanywa; simba wamemfukuzia mbali; kwanza mfalme wa Ashuru amemla, na mwisho Nebukadreza huyu, mfalme wa Babeli, amemvunja mifupa yake. 18Basi, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, mimi nitamwadhibu mfalme wa Babeli, na nchi yake, kama nilivyomwadhibu mfalme wa Ashuru. 19#Isa 65:10Nami nitamleta Israeli tena malishoni kwake, naye atalisha juu ya Karmeli, na Bashani, na nafsi yake itashiba juu ya milima ya Efraimu, na katika Gileadi. 20#Yer 31:34; Isa 1:9Katika siku hizo na wakati huo, asema BWANA, uovu wa Israeli utatafutwa, wala uovu hapana; na dhambi za Yuda zitatafutwa, wala hazitaonekana; maana nitawasamehe wale niwaachao kuwa mabaki.
21 # Isa 10:6 Panda juu ya nchi ya Merathaimu, naam, juu yake, na juu yao wakaao Pekodi; ua, ukaangamize nyuma yao, asema BWANA, ukatende kama nilivyokuagiza, yote pia.
22Pana mshindo wa vita katika nchi,
Mshindo wa uharibifu mkuu.
23 # Isa 16:6; Yer 51:20 Imekuwaje nyundo ya dunia yote
Kukatiliwa mbali na kuvunjwa?
Imekuwaje Babeli kuwa ukiwa
Katikati ya mataifa?
24 # Dan 5:30 Nimekutegea mtego, Ee Babeli, nawe ukanaswa, nawe ulikuwa huna habari; umeonekana, ukakamatwa, kwa sababu ulishindana na BWANA. 25#Isa 13:5BWANA amefungua akiba yake ya silaha, naye amezitoa silaha za ghadhabu yake; maana Bwana, BWANA wa majeshi, ana kazi atakayofanya katika nchi ya Wakaldayo.
26Njoni juu yake toka mpaka ulio mbali;
Zifungueni ghala zake;
Mfanyeni kuwa magofu na kumharibu kabisa;
Msimsazie kitu cho chote.
27 # Zab 22:12; Isa 34:7; Yer 48:44 Wachinjeni mafahali wake wote;
Na watelemkie machinjoni;
Ole wao! Maana siku yao imewadia,
Wakati wa kujiliwa kwao.
28 # Yer 51:10 Sauti yao wakimbiao na kuokoka,
Kutoka katika nchi ya Babeli,
Ili kutangaza Sayuni kisasi cha BWANA, Mungu wetu,
Kisasi cha hekalu lake.
29 # Ufu 18:6; Omb 3:64; 2 The 1:6; Isa 47:10 Waiteni wapiga mishale juu ya Babeli,
Naam, wote waupindao upinde;
Pangeni hema kumzunguka pande zote;
Ili asiokoke hata mtu mmoja wao;
Mlipeni kwa kadiri ya kazi yake;
Mtendeni sawasawa na yote aliyoyatenda;
Kwa sababu amefanya kiburi juu ya BWANA,
Juu yake aliye Mtakatifu wa Israeli.
30 # Yer 49:26; 51:4 Kwa sababu hiyo vijana wake wataanguka katika njia kuu zake, na watu wake wa vita, wote pia, watanyamazishwa katika siku hiyo, asema BWANA.
31Tazama, mimi ni juu yako, Ewe mwenye kiburi, asema Bwana, BWANA wa majeshi; maana siku yako imewadia, wakati nitakapokujilia. 32#Yer 21:14Na mwenye kiburi atajikwaa, na kuanguka, wala hapana atakayemwinua; nami nitawasha moto katika miji yake, nao utawala wote wamzungukao pande zote.
33BWANA wa majeshi asema hivi, Wana wa Israeli, na wana wa Yuda, wameonewa pamoja; na wote waliowachukua mateka wanawashika sana; wanakataa kuwaacha. 34#Ufu 18:8; Mit 23:11; Isa 47:4Mkombozi wao ni hodari; BWANA wa majeshi ndilo jina lake; yeye atawatetea kwa bidii, apate kuistarehesha nchi, na kuwasumbua wakaao katika Babeli. 35#Dan 5:30; Isa 37:13Upanga u juu ya Wakaldayo, asema BWANA, na juu yao wakaao Babeli, na juu ya wakuu wake, na juu ya watu wake wenye hekima. 36Upanga u juu ya hao wajisifuo, nao watapumbazika; upanga u juu ya mashujaa wake, nao watafadhaika. 37#Yer 25:20; 51:30; Nah 3:13Upanga u juu ya farasi zao, na juu ya magari yao ya vita; na juu ya watu wote waliochanganyika ndani yake, nao watakuwa kama wanawake; upanga u juu ya hazina zake, nazo zitaibwa. 38#Isa 44:27; Ufu 16:12; Yer 51:32,36Ukosefu wa mvua u juu ya maji yake, nayo yatakaushwa; maana ni nchi ya sanamu za kuchongwa, nao wameingiwa na wazimu kwa ajili ya sanamu. 39#Ufu 18:2; Isa 13:21; Yer 51:37; 25:12Basi, wanyama wakali wa jangwani, pamoja na mbwa-mwitu, watakaa huko, na mbuni watakaa ndani yake; wala haitakaliwa na watu milele; wala hapana mtu atakayekaa huko tangu kizazi hata kizazi. 40#Mwa 19:24-25; Kum 29:23; Isa 1:9; Yer 49:18; Amo 4:11; Sef 2:9; 2 Pet 2:6; Yud 1:7Kama vile vilivyotokea Mungu alipoangusha Sodoma na Gomora, na miji iliyokuwa karibu nayo, asema BWANA; kadhalika hapana mtu atakayekaa huko, wala hapana mwanadamu atakayekaa huko kama wageni wakaavyo. 41#Yer 6:22; Ufu 17:16Angalia, watu wanakuja watokao kaskazini; na taifa kubwa, na wafalme wengi wataamshwa toka pande za mwisho za dunia.
42 # Isa 13:18; 5:30 Wanashika upinde na mkuki;
Ni wakatili, hawana huruma;
Sauti yao inanguruma kama bahari,
Nao wamepanda farasi;
Kila mmoja amejipanga kama aendaye vitani,
Juu yako, Ee binti Babeli.
43 # Yer 49:24 Mfalme wa Babeli amesikia habari zao,
Na mikono yake imekuwa dhaifu;
Dhiki imemshika, na maumivu,
Kama ya mwanamke katika utungu wake.
44 # Ayu 41:10; Dan 5:2,20 Angalia, atapanda kama simba toka kiburi cha Yordani juu ya malisho yasiyonyauka; lakini nitamkimbiza ghafula ayaache; na yeye aliye mteule nitamweka juu yake; maana ni nani aliye kama mimi? Tena ni nani atakayeniandikia muda? Tena ni mchungaji yupi atakayesimama mbele zangu?
45 # Zab 33:11; Isa 14:24; Yer 51:11; Mdo 4:28; Efe 1:11; 1 Kor 1:27 Basi, lisikieni shauri la BWANA,
Alilolifanya juu ya Babeli;
Na makusudi yake aliyoyakusudia
Juu ya nchi ya Wakaldayo.
Hakika watawaburura, naam, wadogo wa kundi;
Hakika malisho yao yatafadhaika kwa ajili yao.
46 # Ufu 18:9 Kwa mshindo wa kutwaliwa Babeli nchi yatetemeka,
Na kilio chake chasikiwa katika mataifa.

Iliyochaguliwa sasa

Yer 50: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha